HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 18, 2019

MAKAMU WA RAIS AONGOZA UTOAJI WA TUZO ZA I CAN KWA WATU WENYE ULEMAVU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza watu wenye ulemavu kutumia fursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye hafla ya utoaji tuzo ya I CAN kwa watu wenye ulemavu iliyoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Foundation, iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

“Serikali inapenda kuwahakikishia kuwa changamoto za walemavu zinafanyiwa kazi moja baada ya nyingine.”Alisema Makmu wa Rais.

Aidha, Serikali imeendelea kuweka mifumo, taasisi mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha kuwa kuna miundombinu wezeshi ya elimu, afya na teknolojia ili watu wenye ulemavu kuajirika kwenye viwanda vyetu.

“Nitoe rai kwa waajiri na wamiliki wa viwanda kote nchini kuhakikisha kuwa hawabagui wala kunyanyapaa walemavu katika kuijenga Tanzania ya Viwanda ambayo ni jumuishi kwa wote” alisisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua, inathamini na inapongeza jitihada za Dkt. Reginald Mengi pamoja na taasisi yake mpya ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation ambayo pamoja na mambo mengine inahimiza ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika ajira.

Vilevile Makamu wa Rais aliwaambia wananchi waliohudhuria hafla hiyo kuwa Serikali imeweka mkazo maalum katika masuala ya elimu jumuishi ambapo watu wenye ulemavu watasoma vizuri kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.

Kwa Upande mwingine Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amesema Tuzo za I CAN zimekuwa chachu sana kwa watu wenye ulemavu ambapo alimpongeza na kumshukuru Dkt. Reginald Mengi kwa moyo wake wa kipekee wa kutambua na kuwasaidia walemavu.

Aidha, amesema Serikali ina mpango endelevu  wa kutoa elimu ya masuala ya ulemavu ikiwa pamoja na kuendelea kufanya jitihada za kuongeza wakalimani wa lugha za alama.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe amesema sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 inatambua fursa na haki sawa katika kupata elimu hivyo Serikali inaendelea kuboresha miundombinu wezeshi kwa wote wenye mahitaji maalumu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuza ya I CAN pamoja na chakula cha mchana iliyoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Sehemu ya Watu wenye Ulemavu waliohudhuria hafla ya utoaji tuza ya I CAN pamoja na chakula cha mchana iliyoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha juu kitabu cha I Can, I Must, I Will kama ishara ya kuzindua toleo maalum kwa wasioona (kiatu cha nukta nundu) leo wakati wa hafla ya utoaji tuza ya I CAN pamoja na chakula cha mchana iliyoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Balozi wa Marekani Nchini Dkt. Inmi Patterson (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni mbili za Kitanzania Bi. Rehema Said mshindi wa Tuzo ya I CAN ya Mafanikio katika Michezo iliyotolewa na  Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsalimia Bi.Wakonta Kakunda (kulia) ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya I CAN ya Mafanikio katika Ujuzi wa Kipekee kwenye hafla ilioandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya I CAN ya heshima kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation Dkt. Reginald Mengi (kushoto) kwa kutambua mchango wake katika kusaidia watu wenye ulemavu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad