BancABC
kupitia Huduma ya Mkopo Rahisi imejidhatiti kuhakikisha inainua na
kuendeleza mazingira ya elimu katika wilaya ambazo benki hiyo inafanya
shughuli zake kupitia miradi yake ya kusaidia jamii inayowazunguka.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi Bw.
Emmanuel Nzutu alisema wanaunga mkono juhudi za serikali kutoa elimu
bure kwa kila Mtanzania kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
" Hivyo leo sisi kama Bancabc tunatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi, na msaada huu tunaukabidhi hapa kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Sauda Salum Mtondoo.”
" Hivyo leo sisi kama Bancabc tunatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi, na msaada huu tunaukabidhi hapa kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Sauda Salum Mtondoo.”
Alisema
BancABC inaamini katika umuhimu wa Elimu bora ndani ya jamii zetu hapa
Tanzania ,hivyo inaunga mkono Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa
na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Mafuguli,alisema
na kuongeza kuwa katika miradi mbali mbali ya elimu inayofanywa na benki
hiyo lengo lake kuu ni kusaidia kuinua kiwango cha elimu na kuifikia
kila jamii hasa maeneo ya vijijini .
"BankABC inatoa huduma ya Mkopo ambao ni mahususi kwa wafanyakazi wa serikali, Easy loans ambapo inakupa nafasi ya kulipa Mkopo kwa muda wa miaka sita na vile vile una uwezo wa kuweza kuongeza Mkopo hata kabla ya kumaliza kulipa ule wa awali,
Uzuri
wa mkopo huu tofauti na mikopo mingine ni kwamba, mwenye kuomba Mkopo
anaweza kuchagua ni mradi gani wa kuwekeza fedha zake kwa mfano kulipa
karo ya shule, kununua gari, kufanya marekebisho ya nyumba, kulipa kodi
ya nyumba au kumalizia ujenzi,Vile vile tunaweza kununua Mkopo wako wa awali ukabaki na Mkopo mpya",alisema Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi Bw. Emmanuel Nzutu .
Alisema
Mkopo huo utakuwa na bima ya maisha pale ambapo mwenye Mkopo
anapofariki, familia yake itapewa fedha taslimu Tzs 500, 000 kwa ajili
ya kugharamia mazishi.’
"Tunatoa
wito kwa wateja wetu na wale ambao pia sio wateja wetu kujiunga na
Bancabc na kuchangamkia Mkopo huu kwani sisi tunakuweka karibu na ndoto
zako"alimaliza kusema Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi Bw. Emmanuel Nzutu .
Nae mkuu
wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo,wakati akipokea msaada huo
aliishukuru benki hiyo kwa msaada walioutoa wa kuchangia suala la elimu
katika Wilaya yake,aidha pia DC Mtondoo ameikaribisha benki hiyo kutoa
huduma zao mbalimbali kwa Wananchi.
"BancABC tunawashukuru mno kwa msaada wenu mlioutoa,lakin pia tunawakaribisha msogeze pia huduma zenu kwa Wananchi wilayani hapa,ili Wananchi wanedelee kunufaika na huduma zenu mnazozitoa",alisema DC Mtondoo.

Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu
(Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa
wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo
Mwakilishi
wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja
na Asmah Abubakar(kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi
msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo (kulia)

.
Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo, mkuu wa Wilaya ya Kilindi akikabidhi mabati
yaliyotolewa na BancAbc kwa walimu wa shule ambazo zimenufaika na msaada huo.

Mwakilishi
wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja
na Asmah Abubakar kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa
mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo
No comments:
Post a Comment