HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 28 March 2019

Balozi Seif ahudhuria maonesho ya kilimo Cuba

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, na Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dkt. Makame Ali Ussi, wakikaribishwa na Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba Jose Miguel Rodriquez De Armas, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya 22 ya Kilimo yaliyofanyika jijini Havana, Cuba. Balozi Seif Ali Iddi alialikwa kama mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo yaliyofanyika mnamo tarehe18 Machi, 2019. Maonesho hayo yalihudhuriwa na wananchi zaidi ya 3000. 
Balozi Seif Ali Iddi, akitizama kikundi cha wakulima waliokuwa wameandaliwa kutoa burudani kwenye maonyesho hayo. 
Burudani zikiendelea kutolewa na vikundi mbalimbali vya wakulima. 
Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba Jose Miguel Rodriquez De Armas, akihutubia kwenye ufunguzi wa maonyesho hayo. 
Balozi Seif Ali Iddi, akitembelea na kujionea mazao mbalimbali yanayolimwa nchini Cuba kwenye mabanda ya makampuni mbalimbali ya wafanyabiashara na yawakulima.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad