WATUHUMIWA WATATU WA MAUAJI YA WATOTO MKOANI NJOMBE WAFIKISHWA MAHAKAMANI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 12 February 2019

WATUHUMIWA WATATU WA MAUAJI YA WATOTO MKOANI NJOMBE WAFIKISHWA MAHAKAMANI


Jeshi la Polisi Makao Makuu  Kitengo Maalum cha Kupambana na uhalifu kikiongozwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas (pichani), kwa kushirikiana na Jeshi  la  Polisi Mkoa wa Njombe leo tarehe 12/02/2019 limefanikiwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa watatu wa mauaji ya watoto Mkoa wa Njombe
Kati ya hao watuhumiwa ni pamoja na mhusika wa mauaji ya watoto wa familia moja  anayetambulika kwa jina la  Joel Joseph Nziku mwenye umri wa miaka 35 na mkazi wa Magegere,  Makambako
 Inadaiwa Joel Joseph Nziku  alihusika na mauaji ya watoto hao siku ya jumamosi tarehe 19.01.2019 majira ya saa moja jioni, watoto hao ni Godliver Nziku miaka 12, Gasper Nziku miaka 7 na Giliad miaka 5 wote  wakiwa wa familia moja ambao baba yao alifahamika kwa jina la Danford  Nziku miaka 52 mkazi wa kijiji IKando wilaya ya Makambako mkoani Njombe

Aidha Naibu kamishna Sabas amesema kwa sasa  Mkoa wa Njombe na nchi kwa ujumla ni salama na amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano baina yao na Vyombo vya Ulinzi na  Usalama

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad