HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 13, 2019

WASANII WATANO WA KITANZANIA KUSHIRIKI COKE STUDIO AFRIKA 2019

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Msimu Mpya wa Coke Studio Africa umezinduliwa rasmi Tanzania katika halfa iliyofanyika klabu ya burudani Lifepark Mwenge.

Tanzania itawasikilishwa na wasanii watano watakaotumbuiza katika msimu wa sita wa Coke Studio.

Akizungumza mbele ya wageni waalikwa Mkurungezi mkuu wa Coca cola Kwanza Basil Gadzios amekiri kufurahishwa vipaji na uwezo wa wasanii watanzania watakao shiriki kwenye msimu huu mpya.

Kwa upande wake mkurugenzi wa mauzo na masoko wa Cocacola Kwanza, Josephine Msalilwa, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wasanii hao kuwa ni Faustina Charles' Nandy', Raymond Mwakyusa'Rayvanny', Rajabu Abdul'Harmonize', Juma Jux na Mimi Mars.

Amesema wasanii hao wataungana na wasanii wengine 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kutimiza idadi ya wasanii 25 watakaokuwa katika msimu wa mwaka huu.

"Nchi nyingine msanii huchukuliwa mmoja lakini kwa Tanzania imekuwa tofauti kidogo, hii yote inaonesha ni namna gani muziki Watanzania yani bongo fleva umekuwa ukikubalika na wasanii wake kupendwa," amesema Josephine.

Nao wasanii akiwemo Rayvanny amesema anashukuru kuwa mmoja wasanii watakaotumbuiza katika msimu huu huku akieleza hii ni mara yake ya pili.

Msanii Nandy amesema kushiriki Coke Studio 2019 kunakusaidia kukutana na wasanii kutoka Africa wenye vipaji lukuki... nafasi hii kwa msanii yoyote ni kitu cha kujivunia sana na pia inasaidia kutengeneza kazi tofauti na kufanya jina au brand ya msanii kuimarika na nguvu katika soko la muziki Afrika na dunia nzima.

"Coke Studio ni kitu kikubwa, na hakuwahi kutegemea kukutana na msanii mkubwa kama Skales kutoka nchini Nigeria ambaye ameurudia wimbo wake wa Ninogeshe na kunuelezea kuwa ni msanii ambaye ana ushirikiano mzuri," amesema.
 Msanii Hamonize akizungumza katika uzinduzi huo. Wengine ni Rayvan, Jux na Nandy.
 Msanii Nandy akiimba huku akicheza na Mkurungezi mkuu wa Coca cola Kwanza Basil Gadzios wakati wa azinduzi huo.
 Wageni waalikwa wakifuatilia.
 Msanii Jux akitoa burudani.
  Wageni waalikwa wakifurahia.
 Msanii Hamonize akifanyiwa mahojiano na wanahabari.
 Mtangazaji wa Times Redio, Lil Ommy akipata selfie na msanii Jux.
Dj D-Ommy akitoa burudani. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad