HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 13, 2019

Wadau wakutana kujadili mfumo wa kwenda katika Bima ya afya kwa Wote

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Wadau mbalimbali wamekutana kujadili namna ya kwenda katika Bima ya afya ya wote ili kusaidia wananchi kuwa na uhakika wa matibabu.  Wakizungumza katika na waandishi habari jijini Dar es Salaam wamesema kuwa kuwa katika huduma za Afya zinazotolewa na mfuko wa bima ya afya ya Jamii (CHF) umefanikiwa  na sasa kwenda na Bima ya afya kwa kutokana kwa kuandaliwa kwa mswada wa sheria wa bima ya afya kwa wote.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto  na Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Subi amesema kuwa Tanzania imefanya vizuri katika mfuko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa Afrika Mashariki na kufanya watu wengine kuja kujifunza hivyo sasa ni kwenda katika Bima ya afya kwa wote kufikia 2030.
Amesema serikali  imewekeza nguvu kubwa katika sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya ikiwemo  na kuja na Bima ya afya kwa wote.

Dkt.Subi amesema kuwa watu wanaopata huduma za bima ya afya ni asilimia 33 hivyo kwa asilimia 67 iliyobaki itafikiwa katika na Bima ya Afya kwa wote. Amesema vituo vya afya 300 vimejengwa huku vingine vikiwa vimeboreshwa katika kipindi kifupi huku upatikanaji wa dawa muhimu ni asilimia 90 na Hospitali 67 zimeboreshwa. Nae Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma Afya Ofisi ya Rais-Tamisemi  Anna Nswila  amesema kuwa mkutano huo utakuja namna ya kufikia utoaji wa bima ya afya kwa wote na serikali imewekeza katika sekta ya afya katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na uhakika wa matibabu.

Amesema kuwa uchumi wa viwanda unategemea na wananchi kupata matibabu bima ya afya katika kufanya wananchi washiriki katika fursa za uchumi mbalimbali. Kiongozi wa mradi wa Tanzania Health  Promotion (TPH)  Profesa Manoris Meshack amesema kuwa mradi wa CHF umefanikiwa katika mikoa 17 na unaendelea na kwenda hivyo bima ya afya kwa wote utakuwa umejibu changamoto mbalimbali za upatikanaji wa matibabu kwa wananchi.

Amesema kuwa mradi ulikuwa umejikita katika mikoa mitatu ya Singida , Morogoro pamoja na Dodoma na matokeo yake yamekuwa na ufanisi. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu atakuwa mgeni rasmi katika ufungaji mkutano huo wa kwenda katika Bima ya afya kwa wote.
 Kiongozi wa mradi wa TPH , Profesa  Manoris Meshack akizungumza namna mradi ulivyofanikiwa na kuamua kukutana kujadili masuala mbalimbali ya kwenda katika Bima ya afya kwa wote.
 Mkurugenzi Msaidizi  wa Huduma za Afya wa Ofisi ya Rais-Tamisemi Anna Nswila akizungumza namna na wakijipanga katika sera ya kwenda utoaji huduma ya bima ya afya kwa wote.
 Baadhi ya wadau katika mkutano wa kujadili kwenda katika Bima ya afya wote.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto na Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara hiyo Dkt Leonard Subi akizungumza na waandishi habari kuhusiana na wadau kujadili bima ya afya kwa wote katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad