HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 11 February 2019

MTOTO ALIYENUSURIKA KUUAWA NJOMBE AFARIKI DUNIA,AZIKWA

Mtoto Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema Halmashauri ya Mji wa Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo amefariki dunia Februari 09 akiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya alipokwenda kuangaliwa maendeleo ya hali yake.

Mtoto huyo aliokotwa barabarani jirani na porini akiwa amejeruhiwa kwa kukatwa koromeo Desemba 23 mwaka Jana majira ya saa 4 asubuhi mtaa wa mji mwema.

Akizungumza katika mazishi ya mtoto huyo jana katika kijiji cha Ngalanga mjini Njombe, mjomba wa marehemu Gisbeth Mlelwa,alisema marehemu alijeruhiwa na watu wasiojulikana na kupelekwa Hospital ya Mkoa Kibena na kisha kupewa rufaa kwenda Mbeya.

"Marehemu alilazwa na kupatiwa matibabu na baadae Januari 19 mwaka huu aliruhusiwa,na Februari 8 alirudi tena Mbeya kuonana na daktari ambapo Febuari 9 alifariki dunia"alisema Mlelwa.

Akizungumzia tukio hilo lililotokea Desemba 23 mwaka Jana Mwenyekiti wa mtaa wa mji mwema Alanus Mwalongo alisema alipata taarifa kuwa kuna mtoto kachinjwa kutoka kwa Balozi wake.

"Alinipigia simu nikiwa dukani kwangu kwamba mwenyekiti kuna tukio limetokea hapa kanisa la Aglikan kuna mtoto kachinjwa nikawaambia wamlete mje nae huku na walipomleta na mtoto bahati nzuri kuna kijana mmoja alikuwa anapita maeneo akawa amemuona mtoto anatokea porini na kuja barabarani ndiye aliyetoa taarifa"alisema Mwalongo.

Alisema baada ya kumuona mtoto akiwa amekatwa koromeo walimchukua na kumpeleka Hospital ya Kibena ambapo baadae alipata rufaa kwenda mbeya.Mwalongo alisema kwa kishirikiana na Jeshi la Polisi walienda hadi katikati ya msitu alipotokea mtoto na kuliona eneo alilochinjiwa.

"Majira kama ya saa 10 jioni Polisi walinipigia kuwa wanakuja kuona eneo aliloonekana mtoto tuliondoka pale tukaanza kutoka na ule msitu ambao ni viwanja vya Mekson tulipokua tunakwenda kule kijana alipoelekeza tulipokua katikati tukakuta kweli yule mtoto alipolazwa na kufanyiwa unyama ule tukakuta hapa wameweka ndala zake,sweta hapa suruali walimvua nguo zote na barabarani alikutwa uchi"alisema Mwalongo.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio la mtoto huyo Jeni Chanda alisema alimuona mtoto akiwa na kijana akiwa amechinjwa na alipomuuliza alimwambia alimuona anatokea porini akiwa uchi na hivyo alimfunika.

"Mimi nilikua napita ndio nikamuona akiwa na kijana mmoja kutoka na hali aliyokuwa nayo nikachukua nguo zangu nikamfunika ili kumpeleka hospitality"alisema Jeni.Akitoa Salamu za Wizara ya Afya, Maendeelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizarani humo Bi. Mwanaisha Moyo amesema kuwa Wizara inatoa pole kwa familia hiyo na kutoa wito kwa wananchi wa Njombe kuhakikisha wanamlinda mtoto asipatwe na majanga kama hayo.

“Tumesikitishwa na tukio hilo na matukio yote yaliyotokea mkoani Njombe wazazi tuwalinde watoto wetu” alisema.Mpaka sasa vifo vya watoto wadogo kutekwa na kukutwa wakiwa wamechinjwa vimefika nane.
  Ndugu wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake akitengeneza tuta la kaburi mara baada ya mazishi ya mtoto huyo.
 Wanachi wa Kijiji cha Ngalanga wakiwa katika huzuni kubwa mara baada ya kutoka kuuzika  mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake.
 Wanachi wa Kijiji cha Ngalanga wakizika mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake. 
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Njombe Bw. Emmanuel George akiwaongoza wananchi wa kijiji cha Ngalanga kubeba jeneza liliokuwa na mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake.
 Ndugu wakiuaga mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake. 
 Wanachi wa Kijiji cha Ngalanga wakiwa wamebeba  kwenda kuuzika mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad