HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 10 February 2019

MAUJI YALIYOTOKEA YANAZOROTESHA UCHUMI- DC NJOMBE

Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amesema matukio ya utekaji na mauji ya watoto Wilayani Njombe yamesababisha uchumi kuzorota kwa kushuka kwa uzalishaji mali kwa wananchi.

Amesema hali hiyo inatokea kwa kuwa wazazi wanatumia muda mwingi kwapeleka watoto na kuwafuata watoto shule hivyo kupoteza muda na kusimamisha shuguli zao.

Ameyasema hayo jana wakati akifunga maombi katika Kanisa la TAG Milinze yaliyolenga kuombea Wilaya hiyo kuondokana na matukio ya utekaji na mauaji ya watoto.“ Hatuwezi kufikia uchumi wa Viwanda kama matukio haya yataendelea wazazi wanapoteza sana muda katika kuhakikisha watoto wao wanapata ulinzi kwa kuwapeleka na kuwarudisha nyumbani” amesema

“ Niwaambie tu Halmashauri ya Mji wa Njombe inaoongoza katika Halmashauri zote nchini kwa kuwa na kipato kikubwa ana kwa mwaka mwananchi wa hapa ana uwezo wa kuwa na shillingi million 5”

Mkuu wa Wilaya huyo amewataka waumini wa Kanisa hilo na wananchi wa Wilaya na Mkoa wa Njombe kwa ujumla kuombea mkoa wao ili kuondokana na vitendo hivyo vinavyopelekea kuzorotesha shughuli za kiuchumi.

Akitoa salama za Wizara Mwenyekiti wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara za Maendeleo na Ustawi wa Jamii) Bi. Hanifa Selengu amesema Serikali ipo pamoja na wananchi wa Mkoa wa Njombe katika kulaani matukio hayo ya utekeaji na mauaji ya watoto yaliyojitokeza.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri akizungumza na waumini wa Kanisa la TAG Melinze wakati wa kufunga maombi ya kuuombea mkoa wa Njombe kutokana na mauaji ya Watoto yaliyotokea Mkoani Njombe.
Mwenyekiti wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ( Idara za Maendeleo na Ustawi wa Jamii) Bi. Hanifa Selengu akitoa salamu za Wizara kwa waumini wa Kanisa la TAG Melinze wakati wa kufunga maombi ya kuuombea mkoa wa Njombe kutokana na mauaji ya Watoto yaliyotokea Mkoani humo.
Waumini wa Kanisa la TAG Melinze wakimsikiliza MKuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri (hayuko pichani) wakati wa kufunga maombi ya kuuombea mkoa wa Njombe kutokana na mauaji ya Watoto yaliyotokea Mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri (wa Tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waumini wa Kanisa la TAG Melinze na Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ( Idara za Maendeleo na Ustawi wa Jamii mara baada ya kufunga maombi ya kuuombea mkoa wa Njombe kutokana na mauaji ya Watoto yaliyotokea Mkoani humo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad