HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 8, 2019

Mashua ya plastiki yatua Zanzibar, UN yapongeza SMZ kwa kukabili taka za plastiki

 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano-Afrika wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Mohamed Atani (kushoto), pamoja na Mwakilishi wa UNEP Tanzania, Clara Makenya (kulia) wakiongozana na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler (katikati) alipowasili  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe kupitia Mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iliyopo kwenye fukwe za Forodhani visiwani humo. 
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano-Afrika wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Mohamed Atani (kushoto), Mwakilishi wa UNEP Tanzania, Clara Makenya (katikati) pamoja na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler (kulia) wakiwa kwenye chumba maalum cha wageni mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
 Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler (katikati) akitazama zawadi ya shati la kitenge alilokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano-Afrika wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Mohamed Atani (kulia) huku Mwakilishi wa UNEP Tanzania, Clara Makenya akishuhudia tukio hilo katika chumba maalum cha wageni mashuhuri mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

 Mashua iliyotengenezwa kwa taka za plastiki ikiwa imetia nanga kwenye fukwe za Forodhani visiwani Zanzibar iliyofanya safari kutokea LAMU-ZANZIBAR huku njiani ikiendelea na kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe kupitia Mashua hiyo.
 Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler akishiriki zoezi la kusafisha pembezoni mwa fukwe za Serena Hoteli kwa kuokota taka za plastiki ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Wakazi wa visiwani Zanzibar wakiwemo wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na watalii wakishiriki zoezi la kusafisha pembezoni mwa fukwe za Serena Hoteli kwa kuokota taka za plastiki ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikani akishiriki zoezi hilo kwa kuokota taka za plastiki pembezoni mwa fukwe za Serena Hoteli kwa kuokota taka za plastiki ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Wananchi, wakazi wa Zanzibar na watalii wakitazama Mashua ya plastiki iliyotia nanga katika fukwe za Forodhani ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akiagana na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za wizara hiyo visiwani Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akifurahi jambo na Mwakilishi wa UNEP Tanzania, Clara Makenya (kushoto) mara ya mazungumzo na ugeni kutoka UNEA uliofika ofisini kwake visiwani Zanzibar
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler aliyefika ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo. Kushoto ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez aliyeambatana na ugeni huo visiwani Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler aliyefika ofisini kwake visiwani Zanzibar kwa ajili ya kampeni maalum ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika picha ya pamoja na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler na ujumbe aliombatana nao kutoka Umoja wa Mataifa nje ya jengo la Baraza la Wawakilishi visiwani Zanzibar.
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid akizungumza jambo na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi visiwani Zanzibar. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (ZEMA), Sheha Juma.
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid katika picha ya pamoja na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler aliyeambatana na ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa nje ya jengo la Baraza la Wawakilishi visiwani Zanzibar.
 Kikundi burudani cha ngoma ya Kibati kikiimba wimbo maalum wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira wakati wa hafla ya kampeni ya kukabiliana na uchafu wa taka za plastiki baharini na fukwe iliyofanyika viwanja vya Forodhani visiwani Zanzibar.
 Siti and The Band ikitoa burudani ya wimbo maalum unaohamasisha utunzaji wa mazingira unaoitwa “Tudumishe” wakati wa hafla ya kampeni ya kukabiliana na uchafu wa taka za plastiki baharini na fukwe iliyofanyika viwanja vya Forodhani visiwani Zanzibar.
 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wawekezaji wa Sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI), Julia Bishop akitoa salamu za Umoja huo kuunga juhudi za kampeni ya kukabiliana na uchafu wa taka za plastiki baharini na fukwe iliyofanyika viwanja vya Forodhani visiwani Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akisalimiana na Mwanzilishi wa mradi wa Flipflopi –Clean Seas Expedition, Ben Morison wakati wa hafla ya mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iliyotia nanga kwenye fukwe za Forodhani yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe kabla kuelekea kupanda mashua hiyo alipowasili kwenye fukwe za Serena Hoteli visiwani humo. 
 Bidhaa zilizotengenezwa na Plastiki zikiwa kwenye banda la maonyesho wakati wa hafla ya kampeni ya kukabiliana na uchafu wa taka za plastiki baharini na fukwe iliyofanyika viwanja vya Forodhani visiwani Zanzibar.
 Hyuka Hwang kutoka ofisi za UNEP Tanzania akifurahia jambo alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho wakati wa hafla ya mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iluyotia nanga kwenye fukwe za Forodhani yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi visiwani Zanzibar, Ayoub Mahmoud akizungumza machache kabla ya kumrabisha mgeni rasmi wakati wa hafla ya mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iluyotia nanga kwenye fukwe za Forodhani yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akizungumza wakati wa hafla ya mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iluyotia nanga kwenye fukwe za Forodhani yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iluyotia nanga kwenye fukwe za Forodhani yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.

Na Mwandishi wetu
MRATIBU wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez, ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kusimama kidete kupambana na taka za plastiki.
Aidha alisema kutokana na dhamira ya dhati  ya kukabiliana na taka za plastiki taifa hilo linatekeleza mkakati wa kupunguza umaskini na kukuza uchumi wa taifa pamoja na kufikia malengo ya maendeleo endelevu hasa lengo namba kumi na nne la kulinda uhai chini ya maji na lengo namba kumi na tano la kulinda uhai juu ya ardhi.
Mratibu huyo alisema hayo kwenye mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki mjini hapa yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini.
Katika hafla hiyo ambayo viongozi wengi wakiwemo wa serikali walihutubia, Alvaro aliipongeza Tanzania kwa kutenga maeneo ya hifadhi kwa ajili ya manufaa ya wananchi na dunia kwa ujumla na kutia saini mikataba mbalimbali ya hifadhi ikiwamo viumbe wanaotoweka.
Mashua hiyo iliyotengenezwa kwa kutumia mabaki ya plastiki yaliyokusanywa kutoka katika fukwe za Kenya, imeingia nchini juzi ikitokea kwenye mji wa Lamu.
Mashua hii iliyosafiri umbali wa kilometa zaidi ya 500 imesimama katika visiwa kadhaa ili kueneza ujumbe kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya plastiki katika bahari.
Hassan Shafi mmoja wa waliounda mashua hiyo, anasema kilichosababisha ubunifu huu ni uwapo wa takataka nyingi za plastiki ambazo zinapatikana baharini na katika fukwe zinazotishia mazingira ya bahari na viumbe hai.
Alvaro katika mazungumzo yake alisema kutokana na kuzagaa kwa takataka upokeaji wa kampeni ya kusafisha bahari dhidi ya taka za plastiki unaonesha ni kwa namna gani Tanzania ipo tayari kuhifadhi mazingira kwa malengo hayo mawili.
Alisema tatizo la uchafuzi wa bahari limekuwa ni la kidunia na changamoto zake zinaangukia kwa wanaozunguka bahari.
Alisema dunia inatakiwa kuchukua hatua kama Zanzibar za kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki na pia mirija ya kunywea soda, chupa za plastiki na kuendesha kampeni vyombo vya baharini kuacha kutupa uchafu wa plastiki baharini. 
Pamoja na juhudi hizo ametaka kuongezwa kwa jitihada zaidi hasa katika kuelimisha jamii kuchukua jukumu la kutunza mazingira na kupambana na uchafuzi wa plastiki.
Alisema juhudi lazima zifanyike ili kuhakikisha kwamba tishio la kupoteza viumbe wanaoishi baharini katika miaka 30 ijayo linafutwa.
“Utafiti uliofanywa na UNEP unaonesha kwamba dunia itapoteza samaki na viumbe wengine wa baharini miaka 30 ijayo kama kasi ya uchafuzi wa mazingira kwa plastiki utaendelea kama ulivyo sasa” alisema.
Naye Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler ambaye alifika nchini kwa ajili ya hafla hiyo, akizungumza na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Mohamed Abood ofisini kwake Vuga, alisema wananchi wengi wanaozungukwa na ukanda wa bahari wapo hatarini kukabiliwa na magonjwa mbalimbali kutokana na ulaji wao wa  samaki ambao nao wengi huguguna taka za plastiki kama chakula chao cha kila siku.
Alisema watu wengi wamekuwa wakifurahia ulaji wa samaki bila ya kufahamu chakula anachokula samaki kuwa kinaweza kuwa na sumu isiyoweza kuonekana wala kuathiri kwa haraka.
Alieleza katika kujiepusha na mazingira hayo hatarishi jamii haina budi kutunza na kuenzi mazingira ya bahari ikiwemo kuacha tabia ya kutupa taka zote za plastiki katika maeneo ya bahari.
‘’Kuna watu ndani ya jamii yetu hususani wanaoishi kwenye ukanda huu wa bahari wanashindwa kujua kuwa taka zitokanazo na plastiki huweza kudumu hadi kwa miaka 500 baharini bila kuharibika’’aliongezea.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alisema kuna changamoto mbali mbali za utunzaji na uhifadhi wa mazingira visiwani hapa.
Alisema jamii bado ina mwamko mdogo wa kutunza mazingira jambo ambalo amekiri kuwa ni changamoto ambayo inahitaji kusimamiwa ipasavyo.
Hata hivyo alisema anaamini ujio wa mashua hiyo iliyotengezwa kwa taka za plastiki utaleta ujumbe tosha kwa wananchi wa Zanzibar na maeneo mengine kuhifadhi mazingira yao yanayowazunguka.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad