HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 6 February 2019

MAHAKAMA MKOANI TABORA YATAKIWA KUANZISHA MAHAKAMA ZINATEMBEA

NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI Mkoani Tabora imeiomba Mahakama kuanzisha mahakama inayotembelea katika maeneo ambayo hayana huduma hizo ili kuwasogezea wananchi huduma hizo karibu. Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya Sheria nchini.

 Alisema hatua itasaidia kuharakisha utoaji wa haki kwa wananchi wanaoishi mbali na maeneo yenye Mahakama kama vile wilaya ya Sikonge na Uyui. Mwanri aliongeza kuwa zoezi hilo pia litasaidia kusababisha mrundikano wa ksei katika Mahakama ya Tabora.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wanajamii kuwajibika katika kuhakikisha wanawalea watoto wao katika maadili mema ambayo hayatawasababisha kujikuta wakivunja Sheria za Nchi na kukamatwa na vyombo vya dola. Alisema kabla ya jamii kunyoshea kidole Mahakama ni lazima ihakikishe nayo imesimama katika nafasi yake katika kuzuia ovu.

 Mwanri amewataka watendaji hao watimize majukumu yao huku wakijua kwamba mahakama  ndio kimbilio la wanyonge kupata haki. Mkuu huyo wa mkoa aliitaka Mahakama kuhakikisha  maamuzi wanayotoa yawe sahihi ili yasije yakaleta madhara kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Aliwaonya watendaji wake kutojihusisha na vitendo vya Rushwa kwani vitendo hivyo vimekuwa vikilalamikiwa sana na wananchi ambao wamekuwa wakifika katika mahakama kutafuta haki zao.

 Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Salvatory Bongole alisema  kuwa utoaaji haki kwa wakati ni wajibu wa wadau wote. Aliwataka wadau kushirikiana wote wakiwemo Polisi, Mahakimu , Mawakili, Ofisi ya Mwanasheria, Mashahidi na jamii ili kuhakikisha wananchi wanapata haki mapema bila kuchelewa.

 Jaji huyo alisema ucheweshaji wa kesi unachangia kurudisha nyuma maendeleo ya mtu na wakati mwingine Taifa kwa ujumla. Jaji Bongole alisema wadau wakishirikiana na kufanyakazi katika muda unaotakiwa watasaidia kuhakikisha wananchi wanadai haki hawapotezi muda na mali zake wakati wa kufuatilia haki zake.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Askofu mkuu wa kanisa Katoliki jimbo kuu la Tabora Paul Ruzoka amewaasa Majaji na Mahakimu kutoa haki bila ya kupokea shinikizo wakati wanaposikiliza mashauri yanayofikishwa mbele yao na kuyatolea maamuzi.

Kiongozi huyo wa Kanisa katoliki mkoani Tabora amewaomba Majaji na Mahakimu kutotumia mashinikizo ya washauri wa Mahakama bali  watimize wajibu wao kwa haki ili amani iweze kutawala. Katika hotuba yake iliyosomwa na katibu wake Padre Novatus Safari Askofu Ruzoka amewaasa watumishi hao wa Mahakama kutoa Hukumu kwa haki bila ya upendeleo.
 Brass Band ya Chuo cha Ualimu Tabora ikiongoza maandamano ya kuadhimisha siku ya Sheria Mkoa wa Tabora leo
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye suti nyeusi) na Majaji na Mawakili wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya sheria leo.
 Baadhi ya Mawakili mkoani Tabora wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya sheria leo.
 Jeshi la Polisi kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoani tabora  wakiwa katika gwaride maalumu la kuadhimisha siku ya sheria leo
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) akibadilishana mawazo na jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora Julius Malaba(kulia) wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (katikati) akisalimiana na  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Salvatory Bongole (kulia)  na Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Dkt. John Utumwa (kushoto)  wakati wa  kuadhimisha siku ya sheria leo
 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Salvatory Bongole (kulia) akibadilishana mawazo na Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Dkt. John Utumwa (kushoto)  wakati wa  kuadhimisha siku ya sheria leo
  Baadhi ya wakazi wa Manispaa  ya Tabora wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria leo.
 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Salvatory Bongole akitoa hotuba wakati wa   kuadhimisha siku ya sheria leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akihutubia wakazi wa Tabora na wanasheria wakati  kuadhimisha siku ya sheria leo

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad