HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 8, 2019

Klabu tisa kuchuana kuogelea mashindano ya Taliss-IST Jumamosi na Jumpili

 Jumla ya vilabu tisa vimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya Taliss-IST yaliyopangwa kuanza kesho kwenye Bwawa la Kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga Jumamosi na Jumapili.

Meneja wa klabu ya Taliss-IST, Hadija Shebe amezitaja klabu hizo kuwa ni Shule ya Kimataifa ya Moshi (ISM), Wahoo (Zanzibar), FK (Dar es Salaam), ISM (Arusha),  Dar es Salaam Swimming Club (Dar es Salaam), Bluefins (Dar es Salaam) na Mwanza Swimming Club.

Pia katika orodha hiyo, kuna klabu ya Mis Piranhas (Morogoro), Champions Rise (Dar es Salaam) na wenyeji wa mashindani hao, Taliss-IST katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na  DStv, Jubilee Insurance,  Azam, Pepsi, K&K Company, SDS, RK Technotronics, Kaka's Restaurant, Wazazi wa waogeleaji wa klabu ya Taliss-IST  na  Subway Osterbay.

Hadija alisema kuwa vilabu hivyo vinatarajia kuleta zaidi wa waogeleaji 250 ambao watapambana katika umri tofauti. Kutakuwa na kundi la waogeleaji chini ya miaka 8, 9 na 10, 11 na 12, 13 na 14, na zaidi ya miaka 15.

Alisema kuwa mbali ya staili tano za kuogelea, waogeleaji hao watahsindanai katika relei ambayo kwa mtindo wa Individual Medley (IM) na Freestyle. Kwenye IM, waogeaji watachanganya staili nne ambazo ni butterfly, backstroke, breaststroke, na freestyle.

Zaidi ya waogeleaji 250 watashindana katika mashindano hayo ambayo washindi watazawadiwa medali na vikombe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad