HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 15 February 2019

Jopo la Mawaziri Nane lasitisha uhamishwaji wa wananchi katika Bwawa la Mindu

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii Morogoro
Jopo la Mawaziri Nane wametembelea bwawa la Mindu mkoani Morogoro kuangalia namna bora ya sheria ya Usimamizi wa Sh rasilimali za maji  kwa wananchi waliondani ya mita 60 hadi 500 katika Bwawa hilo. Mawaziri Nane hao walifika katika bwawa la maji la Mindu ambalo ndio linalisha maji kwa asilimia 80 katika Manispaa ya Morogoro ambapo kwa sheria hiyo inataka wakazi walioko katika mita zilizo ainishwa kuondoka kwa ajili ya kuepusha madhara kwa wananchi pamoja na kulinda vyanzo vya maji.

Jopo hilo limetokana  na kauli ya  Rais Dkt John Pombe Magufuli kuunda Jopo maalum kwa ajili kuangalia maeneo ambayo yanaingiliana na matatizo ya ardhi na wananchi juu namna bora ya kutoleta madhara kwa wananchi. Mwenyekiti wa Jopo la Mawaziri ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Willam Lukuvi amesema kuwa Mamlaka ya Mkoa yahakikishe inasitisha ujenzi wa makazi katika maeneo ya bwawa la Mindu pamoja kuandika barua kwa waziri mwenye dhamana ya maji ili kutoa kibali cha utekelezaji wa sheria kwa wananchi hao.

Lukuvi amesema utekelezaji wa sheria ya kuwaondoa wananchi isitishwe mpaka waziri atoe kibali.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe  Steven Kebwe amesema wananchi wanatengeneza utaratibu wa kutafuta maeneo ya kuwahamishia katika mpango wa upimaji wa viwanja 3000 na kununua kwa fedha ndogo.  Nae Afisa wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani amesema sheria inakataza wananchi kuingia au kufanya shughuli yeyote katika chanzo cha maji.

Ngonyani amesema kuwepo kwa wananchi katika bwawa la Mindu kumeadhiri kupungua kina cha Bwawa na kuongeza fedha katika kutibu maji  kwa mamlaka ya maji safi ya mkoa huo. Aidha amesema kuwa wanataka kuongeza kingo zaidi katika bwawa hilo huku wafadhili wakitaka kuwaondoa wakazi katika maeneo ya Mindu na Kasanga. Mhandisi Ngonyani amesema kuwepo kwa wananchi hao kuna madhara makubwa ikitokea bwawa hilo kupasuka ambapo hivi karibuni baadhi ya nchi kumetokea kupasuka kwa mabwawa na kuleta madhara makubwa.

"Kuwepo kwa wananchi katika chanzo cha maji ni athari kubwa hivyo maisha ya wananchi na usalama wa afya zao"amesema Ngonyani. Amesema kusitisha baadhi ya shughuli za kibidamu katika bwawa la Mindu kumefanya kupungua kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindu. Jopo la Mawaziri hao watapita katika maeneo  yenye changamoto katika Mikoa Morogoro, Mbeya, Kigoma, Mara, Geita pamoja na Mwanza na kuja na suluhisho bora ya wananchi  katika kuondoa migogoro. Mawaziri hao katika Wizara Ofisi ya Rais-Tamisemi,  Kilimo, Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano - Mazingira,Maliasili na Utalii,Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Ma kazi,Maji pamoja na Mifugo na Uvuvi.
 Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akizungumza uwepo wananchi katika Bwawa la Mindu na madhara ya kuwepo hapo katika Bwawa la Mindu.
 Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi  Simon Ngonyani akizungumza kuhusiana na sheria ya Usimamizi wa Rasilimali Maji ya wananchi kuvamia katika eneo la Bwawa la Mindu.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe akizungumza katika bwawa la Mindu wakati jopo la Mawaziri lilipotembelea Bawawa  hilo.
 Mwenyekiti wa Jopo la Mawaziri , Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na waandishi habari mkoani Morogoro mara baada ya kutembelea Bwawa la Mindu lenye changamoto za kisheria.
Muonekano wa bwawa la Mindu mkoani Morogoro ambalo limevamiwa na wananchi

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad