HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 7, 2019

HALIMA MDEE ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI AKIMUUGUZA MBUNGE MWENZAKE

Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii. 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu,  leo Februari 7, 2019 imeshindwa kuendelea na usikilizwaji wa kesi kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee baada mahakama kupewa taarifa kuwa ameshindwa kufika  kwa  madai kuwa anamuuguza Mbunge Bunda mjini  Ester Bulaya mkoani Dodoma. 

Hayo yameelezwa mdhamini wa Mdee,  Faris Lupomo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa 

Lupomo amedai, aliwasiliana na mbunge huyo na kumueleza kuwa atashindwa kufika mahakamani kwa kuwa anamuuguza mbunge mwenzie Bulaya ambaye anaishi naye Dodoma nyumbani kwake na anamuuguzia Katika hospitali ya Bunge mkoani humo. 

Wakili wa Utetezi Hekima Mwasipu naye alikiri Mahakamani hapo kwa  mshtakiwa huyo hayupo na amepewa taarifa na mdhamini huyo kuwa anamuuguza Bulaya mjini Dodoma. 

Baada ya kusikiliza maelezo hayo, Hakimu Simba amesema, sababu zilizotolewa na mdhamini huyo kuhusiana na kushindwa kufika mahakamani kwa mshtakiwa  zinaleta ukakasi na kubainisha kuwa zina lengo la kuifanya kesi hiyo isimalizike kwa wakati kwa sababu wapo madaktari na wabunge wengine wanawake ambao wanaweza kumuuguza, sasa tukiruhusu haya yaendelee tutashindwa kumaliza kesi. 

"Kiukweli jambo hili linakwaza na linatia wasiwasi kama hii kesi tutaweza kumaliza kwa mwendo huu, tunakubali sababu hiyo ya kuuguza lakini kwa shingo upande, 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi, Februari 28, mwaka huu kwa aji

Mpaka sasa mashahidi watatu wamekwisha kutoa ushahidi katika kesi hiyo akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu wa Polisi Batseba Kasanga.

Mdee anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 3, mwaka jana maeneo ya Ofisi za Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Dar es Salaam ambapo alimtukana Rais Dk John Magufuli kwamba "anaongea hovyohovyo anatakiwa afunge break", kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad