HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 13, 2019

Changamoto za hali ya hewa nchini chanzo cha kuongezeka kwa joto: TMA

Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imesema changamoto mbalimbali za hali ya hewa zinazojitokeza hapa nchini zimesababisha kuongezeka kwa kasi joto nyakati ya usiku ikilinganishwa na mchana.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Utabiri wa TMA, Dk Radslaus Chang'a ameyasema hayo leo Februari 13, katika warsha ya siku moja na waandishi wa habari wakati wakijadili mwelekeo wa msimu wa mvua za masika kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei mwaka huu. Alisema hivi karibuni kumekuwa na changamoto ya hali ya hewa ambayo imekuwa ikijitokeza kwa athari mbaya ya hewa.

Dk.  Chang'a alisema athari mbalimbali zimekuwa zikijitokeza kama kuwepo kwa upepo mkali,mvua kubwa zilizosababisha wananchi kukosa makazi na  kutokea kwa joto kali. "Ingawa majanga ya asili hayawezi kuepukika lakini taarifa zikiwafikia walengwa mapema kabla ya janga kutokea zitasaidia jamii husika, "alisema

"TMA imekuwa ikitoa utabiri wake wa kila siku kwa njia ya televisheni kwa kutumia programu mpya ya teknolojia ya kidigitali ya kisasa,” amesema.
Dk. Chang’a amewaomba wananchi waendelee kufuatilia taarifa za hali ya hewa ili waweze kuchukua hatua stahiki mapema.


Amesema leo watajadili aina mpya ya utabiri wa kila siku kwa watumiaji wa radio lengo lao kusambaza taarifa ili ziweze kuwafikia kwa wakati. Aidha, amezitaka taasisi za maafa pamoja na Serikali kujiweka tayari kukabiliana na madhara yanayoweza kutokea, TMA haina budi kutoa taarifa zake mapema na kwa wakati ili ziwafikie wananchi na sekta husika mapema.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladslaus Chang'a akifungua warsha kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM). 
Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri - TMA, Bw. Samwel Mbuya akiwasilisha mada katika warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Law School of Tanzania Mawasiliano jijini Dar es Salaam. 
Mtaalamu (Utabiri) wa Hali ya Hewa, Elias Lipiki akiwasilisha mada kwa wanahabari katika warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Law School of Tanzania Mawasiliano jijini Dar es Salaam. 
Mwanahabari Faustin Shija kutoka Nipashe, akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA. 
Jerome Mshanga wa Clouds Media akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA kwenye warsha hiyo. 
Mwanahabari na Bloga, John Bukuku akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladslaus Chang'a akifafanua jambo kwenye warsha kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad