HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 15 February 2019

CDF YAKABIDHI KITUO CHA KUTOA HUDUMA ZA UKATILI WA KIJINSIA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
Katibu mkuu wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt John Jingu amezindua rasmi kituo cha kutoa huduma kiitwacho (one stop center)  kwa wanawake na watoto waliofanyiwa ukatili  wa  kijinsia katika hospitali ya Mwananyamala iliyopo wilayani Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi wa kituo hicho umefanyika  wakati Jukwaa la Utu wa mtoto (CDF) likikabidhi jengo hilo katika hospitali ya Mwananyamala kwa Iengo la kusaidia wahanga wote wanaoteseka na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambao hawana sehemu faragha ya kukimbilia kwa ajili ya kueleza matatizo yao.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo katika hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam Katibu mkuu wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto DKT John Jingu ambaye ndiye mgeni rasmi amesema kuwa ni jambo zuri kuanzisha sehemu maalumu za kutoa huduma Kama hizo katika jamii ili iwasaidia walengwa wa majanga hayo kufika mahali ambapo wataweza kuzungumza kwa uhuru bila kuhofia.

" kituo hiki  kitakuwa huru kuhudumia wahanga wa ukatili wa kijinsia hasa wakinamama na watoto ambao wao mara nyingi wamekuwa wakiogopa kwenda mahospitalini kutoa taarifa juu ya ukatili Huo wakihofia sehemu wanayokwenda kueleza matatizo yao hayako  faragha kwao" amesema  DKT Jingu.

Aidha dkt Jingu amesema  kuwa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF)  wameliona hilo kuwa ni tatizo ndio manaana wamefungua kituo hicho kwa ajili ya kusaidia jamii kwa ujumla, na tutaendelea kufungua vituo vingine vya kutoa huduma hiyo hapa nchini"

Vilevile Afisa utamaduni na utawala Mwananyamala Hospitali Mansour Carama amesema kuwa kuwepo kwa kituo hicho Itarahisisha utendaji wa kazi kuwa mzuri na  anaamini kesi zote zitashughulikiwa kwa wakati.

"Kwa kuwa kesi nyingi zimekuwa haziripotiwi na jamii imekuwa ikiumia bila kupata msaada wowote, kutokana na hili pia tunaomba uwepo na utaratibu wa kutoa elimu mara kwa mara kwa ajili ya watu ili wawe na uelewa mpana kutokana na ukatili wa kijinsia"amesema Carama.
 Katibu mkuu wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt John Jingu akizungumza wakati wa makabidhiano ya kituo cha huduma ( one stop  center)  kwa wanawake na watoto waliofanyiwa vitendo vya utili wa kijinsia katika hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt John Jingu akikata utepe akiashiria uzinduzi wa jengo la kutoa huduma  (one stop center)  kwa wanawake  na watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia katika hospital ya Mwananyamala.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad