HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 7 February 2019

ACB WAJIZATITI KUWAINUA KIUCHUMI WAJASIRIAMALI WADOGO NA WA KATI KWA MWAKA 2019

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BENKI ya Akiba Commercial (ACB)   imejizatiti katika kuwainua wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs) kwa kuwapatia mikopo nafuu na ya muda mrefu.

Hayo yalisemwa wakati benki hiyo wakitangaza matokeo mazuri ya fedha ya nusu ya pili ya mwaka 2018 kwa kupata faida ghafi yaani Pre-tax ya Bilion 1.2 ikiwa ni katika ukuaji wa asilimia 600 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2017.

Akizumgumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ACB Augustine Akowuah amesema anafarijika na matokeo hayo ya nusu ya pili ya mwaka 2018 kwani mizania ya malengo yao kuanzia mwaka yamesababisha kuwa na muelekeo mzuri wakati wakifungua mwaka.

Amesema kuwa, wamefurahi hatua hiyo kwa kuwa mikakati mingi waliyojiwekea imeleta mabadiliko kwenye benki yao kwa muda mrefu japokuwa hali haikuwa nzuri mwanzoni mwa mwaka.

"Katika kipindi cha mwaka 2018, ilitelekeza mikakati ya kupunguza mikopo chechefu, kuimarisha makusanyo ya madeni sugu na utoaji wa mikopo mipya kwa kuzingatia ubora, hatua tulizochukua ikiwemo kunadilisha na kupitia majukumu ya kazi zililenga zaidi kwenye kuimarisha hatari zinazotokana na ukopeshaji,"amesema Akowuah. 

Afisa Biashara wa ACB, Felician Girambo amesema kuwa benki hiyo kwa mwaka huu 2019 wamejizatiti kuendelea na matokeo chanya kwani wamelenga kujenga maendeleo chanya yaliyopatikana kwa mwaka 2018 ikiwemo jukumu pekee la kusaidia wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs) nchini Tanzania kwa kutumia huduma bora za kifedha.

Girambo amesema mjasiriamali yoyote mwenye leseni ya biashara ana uwezo wa kupata mkopo hata kama hatakuwa na akaunti katika benki yao ila itamlazimu afungue kwa wakati huo, pia amesema mjasiriamali itamtaka awe na msingi utakaokuwa mara ya mbili ya mkopo anaohuitaji kwa wakati huo.

Ameongezea kuwa, kwa mwaka 2019 wamedhamiria kufikia lengo la kuwapatia mikopo wajasiriamali  12,000 kwa mwaka mzima na mikopo yao inarejeshwa kulingana na aina ya mkopo uliochukua.

Benki hiyo ina jumla ya miaka 20 toka kuanzishwa kwake na ina matawi 18 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Moshi na Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji Benki  ya Akiba Commercial (ACB) Augustine Akowuah akizungumzia matokeo mazuri ya fedha ya nusu ya pili ya mwaka 2018 kwa kupata faida ghafi yaani Pre-tax ya Bilion 1.2 ikwia ni katika ukuaji wa asilimia 600 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2017.
Afisa Biashara wa Benki ya Akiba Commercial (ACB)
, Felician Girambo akizungumzia mikopo kwa 
 wajasiriamali wadogo na waka kati (MSMEs) nchini Tanzania kwa kutumia huduma bora za kifedha.
Meneja Mkuu Kitengo cha Fedha wa Benki ya Akiba Commercial (ACB) Bertha Simon akielezea mikakati waliyojiwekea katika mwaka 2019 ya kuhakikishia wanafikia malengo yao.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad