HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 7, 2019

ZOEZI LA UGAWAJI WA VITAMBULISHO KWA WAJASIRIAMALI LAMALIZIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKOA wa Dar es Salaam umemaliza zoezi la utoaji wa vitambulisho kwa wajasriamali na kuwa kinara kwa kutimiza agizo la Rais  Mh Dkt. John  Magufuli la kutoa vitambulisho hivyo bure kwa wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) kwa nia ya kurasimisha sekta hiyo Muhimu katika ujenzi wa Taifa.

Zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho 25,000 kwa awamu ya kwanza limekamilika  tarehe Januari 3 mwaka huu na kuufanya Mkoa huu kuwa Mkoa wa kwanza kitaifa katika kukamilisha zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo. Baada ya kukamilisha zoezi hilo kwa haraka jijini Dar es Salaam tayari wamepokea  vitambulisho vingine 25,000 kwa ajili ya kuendelea kwa ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa awamu ya pili.

Akizungumza katika makabidhiano ya vitambulisho hivyo kwa wakuu wa wilaya wa Mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemshukuru Rais Magufuli  kwa kukubali ombi la nyongeza ya vitambulisho vingine 25,000 kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar es Salam na kueleza kuwa ugawaji wa vitambulisho hivyo utaanza ambavyo vitaanza kugaiwa katika wilaya zote kuanzi kesho.

 Makonda amesisitiza ufuatajwi wa sheria na kanuni katika ugawaji wa vitambulisho hivyo na kusisitiza kuwa vitambulisho hivyo haviuzwi bali kiasi cha shilingi  20,000 inayotolewa na wafanyabiashara wadogo ni mchango wa gharama za utengenezwaji  na si vinginevyo, na amekemea vikali ulanguzi wowote ambao unaweza kutokea katika zoezi hili la ugawaji.

Vitambulisho hivyo vimekabidhiwa kwa wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam na kupokelewa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kwa niaba yao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (kushoto) akimkabidhi kasha la vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo Mkuu wa Wilaya wa Temeke Felix Lyaniva (kushoto) katikati ni katibu tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Abukar Kunenge.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad