SHINDANO la
Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass'
linalojulikana kama 'MastaBata', leo limeendelea kuchezeshwa huku wateja
sita wakijishindia simu janja za kisasa 'Samsung S9+' zenye thamani ya
shilingi milioni 2,300,000/- kila moja.
Katika
droo hiyo ya nne pia wateja 20 wengine wa benki hiyo wamejishindia
fedha taslimu shilingi 100,000/- ambazo zitaingizwa kwenye akaunti zao
moja kwa moja ndani ya saa 24 tangu kuchezeshwa kwa droo hiyo. Droo hiyo
ya nne iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam imefikisha wateja 80
hadi sasa ambao wameshindia kiasi cha shilingi 100,000/- kila mmoja.
Akizungumza
na wanahabari mara baada ya kuchezeshwa droo ya leo, Meneja Mwandamizi
kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Manfredy Kayala alisema mbali
na droo hiyo kupata washindi 20 wa shilingi 100,000/- kila mmoja, wateja
6 wengine wamejishindia simu aina ya Samsung S9+' kila mmoja yenye
thamani ya shilingi milioni 2,300,000/-.
Alisema
wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja
wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB
Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia zawadi hizo.
Hata
hivyo, aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani
kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100
wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika na shindano
hilo.

Meneja kutoka kitengo cha Kadi cha Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa (kulia) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Droo ya nne ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Katikati ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Semvua akisimamia droo hiyo na Domitila Silayo wa NMB (kushoto).

Mtaalam kutoka kitengo cha Kadi cha NMB, Domitila Silayo (kulia) akiwasiliana na mmoja wa wateja wa NMB waliojishindia simu janja za kisasa 'Samsung S9+' yenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kwenye droo ya nne ya Shindano la MastaBata. Katikati ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Semvua akisimamia droo hiyo pamoja na Sophia Mwamwitwa wa NMB akishuhudia (kushoto).
Meneja Mwandamizi kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Manfredy Kayala akizungumza na waandishi wa habari kufafanua wateja walivyojishindia zawadi anuai kwenye Masta Bata ya NMB.

No comments:
Post a Comment