HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 15, 2019

WANANCHI VISIWANI ZANZIBAR WACHANGAMKIA HUDUMA KWENYE BANDA LA MAONYESHO LA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA


Wananchi wa Tanzania Zanzibar wameendelea kujitokeza kwa wingi kupata huduma za Usajili Vitambulisho vya Taifa zinazotolewa na NIDA wakati wa maonyesho yanayoendelea sambamba na maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar. Pamoja na huduma za Usajili, huduma nyingine zinazoendelea kutolewa kwenye banda hilo ni uchukuaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa waliokamilisha taratibu za Usajili na uhakiki, elimu kuhusu Vitambulisho vya Taifa na  matumizi mapana ya Vitambulisho hivyo katika huduma mbalimbali nchini. 

Sherehe hizo ambazo huambatana na Maonyesho ya Biashara ya kimataifa ambayo yanafanyika katika viwanja vya Maisara vilivyopo mjini Unguja, hufanyika kila mwaka ifikapo Januari. Maonyesho hayo ambayo yameanza tarehe 2/01/2019 yameendelea kuwavutia wananchi wengi kufika katika banda la NIDA; ambapo zoezi la ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa limeonekana kuwagusa wananchi wananchi wengi wakiwemo wale ambao hawakujisajili. 

Wakizungumza baada ya kupata huduma kwenye banda hilo, wananchi wengi wameisifu NIDA  kwa kuwasogezea huduma pamoja na kufanya kazi mpaka muda wa usiku na kutoa fursa kwa wananchi wengi kushiriki na kuweza kunufaika na huduma hiyo.Mamlaka inaendelea kuwakaribisha wananchi wote wanaoishi visiwani Zanzibar kuendelea kufika katika banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ili kuweza kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali za Usajili na Utambuzi zinazotolewa na Mamlaka. Huduma hizo hutolewa kuanzia mida ya saa 4 asubuhi hadi saa 4 usiku kila siku wakati wa maonyesho. 
Afisa Usajili NIDA Salma Shaban Abdallah, akiwapatia maelezo baadhi ya wageni wakazi wanaoishi Visiwani Zanzibar walipofika kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na NIDA katika banda la Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Maisara mjini Unguja.
 Baadhi ya wananchi visiwani Zanzibar wakiwa katika banda la NIDA wakati wa siku ya maadhimisho ya Mapinduzi wakijionea na kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NIDA katika banda hilo. Zoezi hilo limefanyika wakati wa Maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya Maisara.
 Afisa usajili NIDA Salma Shaban Abdallah, akijaza taarifa za mmoja wa wananchi wakati wa kukamilisha zoezi la kumpatia Kitambulisho cha Taifa mwananchi huyo aliyefika katika banda la NIDA kuchukua kitambulisho chake cha Taifa kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Maisara visiwani Zanzibar.
Afisa Habari NIDA Zanzibar, Bw. Said S. Said akiwafafanulia jambo  wananchi waliofika kutembelea banda la maonyesho la NIDA wakati maonyesho ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar yanayoendelea kwenye viwanja vya Maisara Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad