HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 22 January 2019

WANANCHI MANONGA WAMSHUKURU RAIS DKT. MAGUFULI KWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA KULETA MAENDELEO MANONGA

*Gulamali azishukuru  TAMISEMI na Wizara ya Elimu kwa kutoa shilingi milioni 480 kwa sekta ya Elimu.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MBUNGE wa Manonga Seif Gulamali kwa niaba ya wananchi wa jimbo la manonga na Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ametoa shukrani za dhati kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kuunga mkono jitihada za maendeleo nchini na kwa jimbo la Manonga.

Gulamali amesema kuwa uongozi wa awamu ya tano chini Rais Magufuli umegusa maisha ya watu wengi sana wakiwemo wana Manonga ambapo sekta za afya, barabara, elimu, kilimo na viwanda zimeimarika zaidi na ujenzi wa taifa upo katika kasi ambayo manufaa yake ni kwa kila mmoja.

Amesema kuwa wanamanonga wanamtakia Rais Magufuli afya njema na kulipeleka taifa mbele zaidi. Wakati huo huo Gulamali ameishukuru TAMISEMI na Wizara ya Elimu kwa kutoa jumla ya shilingi milioni 480 kwa ajili ya kuimarisha sekta ya Elimu jimboni humo.

Amesema kuwa shule ya Sekondari Choma ilipata jumla ya shilingi milioni 190 ambazo zilitumika katika ujenzi wa madarasa mawili na mabweni mawili. Pia katika shule ya Sekondari ya Mwisi mawili shilingi milioni 190 zilitolewa ambazo zilitumika katika ujenzi wa madarasa mawili na mabweni , na kuweza kuchukua wanafuzi wengi zaidi.

Pia shule ya Sekondari Ziba imepata shilingi milioni 100 ambazo zimetumika katika ujenzi wa bwalo la chakula.

Gulamali amewahakikishia wanamanonga kuwa nguvu iliyopo katika kuboresha sekta za Elimu, Afya na miundombinu haitalega na amewataka kuwa na umoja na ushirikiano katika kuleta maendeleo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad