HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 16, 2019

WAAJIRI WATAKAOSHINDWA KUWASILISHA VIELELEZO VYA RUFAA ZILIZOKATWA NA WATUMISHI WA UMMA KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Tume hiyo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo akieleza majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Tume chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Makao Makuu ya Tume hiyo yaliyopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani)  wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya Tume hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo akifafanua jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Tume chenye lengo la  kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya Tume hiyo yaliyopo Ubungo Plaza  jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu, Dkt. Steven Bwana, akifafanua majukumu ya bodi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya Tume hiyo yaliyopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo akielezea mchakato wa kushughulikia rufaa kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) aipotembelea moja ya ofisi zinazofanyia kazi rufaa zinazowasiliswa Tume ya Utumishi wa Umma. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Umma, mara baada ya kumalizika kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi  wa Tume hiyo cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya Tume hiyo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Waajiri na Mamlaka za Ajira nchini watakaoshindwa kuwasilisha vielelezo vya rufaa zilizokatwa na watumishi wa umma  kwenye Tume ya Utumishi wa Umma ndani ya siku 14 kama sheria inavyoelekeza watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuikwamisha Tume ya Utumishi wa umma kutekeleza jukumu lake la kushughulikia kwa wakati rufaa za watumishi. 
Tahadhari hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma  Makao Makuu ya Tume hiyo, akiwa katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu kwa kina majukumu ya Tume na kujiridhisha namna Tume  hiyo inavyotekeleza majukumu yake.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, kitendo cha waajiri kutowasilisha vielelezo vinavyohitajika na Tume ya Utumishi wa Umma kwa wakati ili kuiwezesha Tume kufanya maamuzi sahihi ya rufaa  imekuwa ni kikwazo cha utekelezaji wa majukumu ya Tume, ambayo moja ya jukumu lake ni kusimamia, kufuatilia na kutathmini uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Utumishi wa Umma nchini.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameisisitiza Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Umma  kuhakikisha inatoa elimu kwa umma kuhusu utaratibu wa kufanyia kazi rufaa zinazowasilishwa ili waweze kujua ni muda gani unaotumika kushughulikia rufaa zao, na kuongeza kuwa elimu hiyo itapunguza malalamiko dhidi ya Tume kuwa haifanyii kazi rufaa zao kwa wakati.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameelekeza kuwa, kuanzia sasa ni marufuku kwa mwajiri yeyote kumhamisha mtumishi aliyebainika kuwa na kosa  mahala pa kazi, kwasababu Tume ya Utumishi wa Umma itashidwa kushughulikia suala la mtumishi huyo na kuna uwezekano mkubwa akafanya tena makosa yale yale anakohamia. 

Kwa upande wake, Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo amesema kuwa, majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma yameainishwa katika Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298  Kifungu 10 (1) ambapo imepewa mamlaka ya kutoa miongozo na kuhakikisha Utumishi wa Umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu. 

Bw. Odongo ameendelea kufafanua kuwa,Tume ya Utumishi wa Umma ni mamlaka ya rufaa kwani inapokea na kushughulikia rufaa za watumishi wa umma, hivyo inafanya kazi kama mahakama ndani ya Utumishi wa Umma na ni chombo cha kutoa haki kwa watumishi wanaoonewa, na kuongeza kuwa, Tume inasimama kama mdhamini kuhakikisha haki inatendeka pande zote yaani kwa mwajiri na mtumishi.

Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu, Dkt. Steven Bwana, amemshukuru Dkt. Mwanjelwa kwa maelekezo ya kuboresha utendaji kazi aliyoyatoa na kuahidi kusimamia utekelezaji wake.
Tume ya Utumishi wa Umma iliundwa kwa Mujibu wa Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 2008 ili kuhakikisha kuwa, Utumishi wa Umma unakuwa mmoja na watumishi wote wanakuwa na taratibu za usimamizi, hadhi, haki na masilahi yanayofanana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad