NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdalah Hamis Ulega ametoa mafuta ya diesel Lita 1000 kwa ajili ya greda ambalo husaidia kutatua changamoto za barabara jimboni humo pamoja na shuka 100 kwa kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.
Akizungumza katika mkutano wa kufunga mwaka wa kutathimini changamoto na maendeleo uliofanyika wilayani humo, Ulega amesema kuwa ameamua kutoa mafuta changamoto iliyotokana na Halmashauri kununua greda muda mrefu lakini limekaa bila kufanya kazi.
"Nilitoa msukumo kwa kukaa pamoja na madiwani na kushauriana kwa pamoja tuwe na greda letu wenyewe ili itusaidie kutatua changamoto za barabara hasa za vijijini ambako barabara nyingi hazipitiki na tumenunua greda hilo kwa zaidi ya milioni 700 ikiwa ni fedha zetu wenyewe na likachonge barabara zetu." Amesema Ulega.
Ulega amesema kuwa greda hilo alikodishwi kwa wananchi ila kinachotakiwa vijiji vijichangishe wanunue mafuta kwa shughuli za kutatua kero za barabara. "Sio kwamba nimeshindwa kutoa hela Mkurugenzi hela nakukabidhi mapipa haya matano ya mafuta kila moja lina Lita 200 yakatumike ipasavyo."Amesema Ulega.
Aidha Ulega ameongeza kuwa shuka mia moja alizozitoa ni kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Mkuranga na hiyo ni kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusiana na uchafu wa mashuka hospitalini hapo. Hamduni Mohamed Ally ni mmoja wa wawekezaji Wilyani humo na kwa upande wake amemuunga mkono Mbunge huyo kwa kutoa shuka hamsini zenye thamani ya zaidi ya laki tano kwa ajili ya hospital hiyo ya wilaya Mkuranga.
"Afya bora inaendana na mazingira ya kutolea huduma na ili mgonjwa awe na afya njema anatakiwa kulala sehemu safi,kuepuka kuambukizana magonjwa mapya." ameeleza Hamduni Nao baadhi ya wananchi wakizungumza kwa niaba ya wenzao wamemshukuru mbunge wao kwa msaada huo,na kutoa wito kwa kwenye mamlaka kutumia fedha katika malengo yaliyokusidiwa.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akikabidhi shuka 100 Mkurungenzi wa Halmashauri Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde zenye thamani zaidi ya milioni moja.kushoto ni Mganga Mkuu wa wa wilaya ya
Mkuranga, Dkt.Stephen Mwandembo
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akimsikiliza Mzee Athuman Mtalu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mkuranga mko wa Pwani.
Mkurugenzi wa Halmashauri Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza na wananchi katika mkutano wa kufunga mwaka wa kutathimini changamoto na maendeleo uliofanyikawa wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Sehemu ya wananchi wakimsiki Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega akikabidhi jezi za mpra seti 14 kwaajili timu mbalimbali za wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment