HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 10 January 2019

Tanzania Kutoa Taarifa Kuu ya Malengo Endelevu 2030, Julai Mwaka Huu

Tanzania inatarajia kutoa taarifa ya takwimu ya malengo endelevu ya dunia 2030 Julai mwaka huu, huku suala la elimu likipewa kipaumbele katika taarifa hiyo. Akizungumza Jijini Dar es Salaam kwenye mkutano na wadau wa takwimu kutoka Sweden, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt Albina Chuwa amesema kuwa lengo kuu lililowakutanisha na wadau hao ni kutoa taarifa kuhusu taarifa kuu ya malengo endelevu ya dunia ya mwaka 2030.

“Huu mkutano lengo lake kuu ni kuwapa wananchi taarifa ya maendeleo ya utengenzaji wa kanzi data ya takwimu za kuripoti katika malengo endelevu ya dunia ya mwaka 2030 ambayo inatarajia kuwekwa hadharani Julai mwaka huu”, Alisema  Dkt.Chuwa. Dkt Chuwa alisema kuwa utengenezaji wa kanzi data hii umeanza muda mrafu kwa Ofisi ya Takwimu ikishirikiana na mtaalamu kutoka Sweden (Alexandra Silfverstolpe) ambaye anafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Ofisi ya Takwimu nchini humo.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilipata uzoefu wa kutengeneza kanzi data hii kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Colombia   kwa kuwa kanzi data hizo zinaonyesha namna ya kutatua matatizo ili kutimiza malengo endelevu kwa taifa.“Kanzi data hii inaonyesha  viashiria kwenye malengo endelevu kwa mfano viashiria vya namna gani Tanzania itaondokana na umasikini ifikapo mwaka 2030, kwa hiyo ni rahisi kwa watu wanaotekeleza sera, wanasiasa na watawala wanaotoa maamuzi katika uchumi wa nchi kwani kanzi data hizi zitawasidia katika kazi zao”, Alisema Dkt. Chuwa.

Aidha aliongeza kuwa shabaha kubwa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu ni kushirikisha wadau wa maendeleo katika kuweka Takwimu sawa kwa  hiyo mkutano wa Ofisi ya takwimu na wadau wa Takwimu  kutoka Sweden  wamejadili pamoja hatua ya utengeneza kanzi data na kutoa kipaumbele malengo enedelevu ya mwaka 2030 katika  sekta ya elimu.

“kwa sasa kazi hii imefikia kwenye hatua nzuri ya kuingiza data kutoka kwenye kanzi data kuziweka kwenye Taarifa kuu inayotarajia kutolewa Julai mwaka huu, kwa hiyo tutafanya kazi hii karibu sana na hawa wenzetu ili kutoa taarifa yenye kiwango cha kimataifa”, Alisistiza Dkt.Chuwa.
Akizungumzia marekebisho ya sheria ya takwimu, Mkurugenzi huyo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu aliwatoa wasiwasi wananchi kuwa hakuna mtu yeyote atakayefungwa kwa kufuata taratibu za utoaji takwimu kwa kutumia data kamili kwani nchi zote duniani zinahitaji data zenye kufuata utaratibu.
Mwisho.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad