HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 8, 2019

TAMADUNI ZENYE MADHARA ZALETA ATHARI KWA WANAWAKE MKOANI MARA

Na Anthony Ishengoma-Mara.
Jamii mkoani Mara bado inaendeleza mila potofu ya kuamini kuwa mwanamke asiyekeketwa ni mkosi kwa familia jambo ambalo linaendeleza vitendo vya kwa ukatili wa hali ya juu dhidi ya wanawake Mkoani humo.

Akiongea wakati wa ufanguzi wa Kikao kazi cha uzinduzi wa Kampeini ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto   leo Mkoani Mara Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Karolina Mtaphula amesema inapotokea binti anayekeketwa akapoteza maisha kutokana na ukeketaji binti huyo amekuwa akitupwa polini bila kuzikwa kwa taratibu za kawaida kwasababu jamii pia inaamini ni mkosi kwa jamii na kwa familia yake.

Aidha Mtapula aliongeza kuwa Jamii ya Mkoa wa Mara inatakiwa ijilinganishe na mikoa mingine ambayo haina mila ya ukeketaji ili kujenga ufahamu kuwa wanawake kutoka jamii hizo kama wamekuwa wakileta mikosi katika familia zao kama amabavyo mila zao inawafanya waamini.

‘’Wanawake katika Mikoa ambayo haina ukeketaji wanazidi kupiga hatua za kimaendeleo na kufaidika kielimu lakini katika Mkoa wa Mara mila potofu imeendelea kurudisha nyuma maendeleo ya wanawake hivyo nawaomba mlinganishe na jamii hizi kuona kama kweli wanawake wasipokeketwa wanaleta mikosi’’. Alendelea kusema Mtapula.

Aidha Mtapula alisema pamoja na kuwepo kwa vitendo vaya ukatili amesema vitendo hivyo katika Mkoa wa Mara takwimu zilizopo zinaonesha vitendo vya mkoani humo vimeanza kupungua kwani kwa takwimu za mwaka 2010 mkoa huo uliongoza kitaifa kwa kuwa na sailimia 72 lakini kwa takwimu za mwaka 2015-216 takwimu zinaonesha mkoa umeshuka hadi kufikia asilimia 55.

Wakati huo huo Mkurugenzi anayeshugulikia masuala ya watoto Sebastian Kitiku amewaambia wajumbe wa kikao kazi hicho kuwa wizara iko mkoani humo kukutana na kujadiliana na viongozi wa Mkoa na Halmashauri pamoja na viongozi wadini kwa ajili kutengeneza ujumbe utakaotumika katika kampeini ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.

Amewataka wajumbe hao kutengeneza ujumbea amabao kimsingi utaendana na mazingira ya Mkoa ikiwemo mila nzuri zilizopo kwakuwa ujumbe unatumika Mazingira ya Mara unaweza usitumike katika mikoa mingine kutokana na tofauti za kimazingira.

Kazi ya kutengeneza ujumbe kwa ajili ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni inaendelea itaendelea katika mikoa yenye takwimu za juu katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambayo ni mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida na Rukwa.    
 Katibu Tawala Mkoa wa Mara Karolina Mtaphula akitoa hutuba yake wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kinachoendelea Mkoani Mara kuandaa ujumbe utakaotumika katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
 Katibu Tawala Mkoa wa Mara Karolina Mtaphula (katikati)  akifuatilia wakati wa kikao kazi cha kuandaa ujumbe utakaotumika katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kulia ni Grace Mwangwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii na kushoto kwake ni Edward Litunda pamoja na Emanuel Kisongo viongozi waandamizi wa Ofisi ya Mkoa wa Mara.
 Baadhi ya Wajumbe wakiwa tayari kwa maandalizi ya  ujumbe utakaotumika katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto leo Mkoani Mara.
Afisa Maendeleo ya Jamii  Mkoa wa  Mara  Neema Ibamba akitoa maelezo wakati wa  kuandaa ujumbe utakaotumika katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Wajumbe wakikao kazi cha kuandaa ujumbe kwa ajili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Mara Karolina Mtaphula akitoa mara baada ufunguzi wa kikao kazi leo Mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad