Muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi amezindua Maktaba ya Shule ya Msingi Tandale Magharibi na kutoa wito kwa wanafunzi kuitumia vyema maktaba hiyo kujenga maarifa.
Aidha amewataka wanafunzi kuilinda maktaba hiyo kama chanzo cha maarifa na weledi.
Maktaba hiyo imewezeshwa na taasisi hiyo kufuatia shindano la Andika Chalenge kwa shule za serikali nchini.
Aliwataka pia wazazi kutekeleza jukumu lao la kushawishi watoto kusoma vitabu na kutumia maktaba na kuwa weledi katika masomo kwa kujisomea.
Akizindua maktaba hiyo ambayo Taasisi iliikarabati, kuweka mashubaka pamoja na vitabu vya aina mbalimbali, Mwenyekiti wa Taasisi, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi amesema amejisikia furaha kutimiza ahadi ya kukabidhi maktaba kwa shule hiyo iliyotoa mshindi.
Katika shindano hilo la uandishi la Andika Challenge ambalo linafanyika mikoa yote Tanzania na kushirikisha wanafunzi wote wa shule za msingi za serikali kuanzia darasa la 4 mpaka la 7 ambapo wanafunzi huandika hadithi na kutuma kwa sanduku la posta 163 Dar es salaam, washindi huzawadiwa tuzo na shule aliyotoka husaidiwa kuwa na maktaba.
Shule ya Msingi Tandale Magharibi imepata maktaba hiyo baada ya mwanafunzi wake Nuurat Venance kushinda shindano la kutunga hadithi lililowashindanisha wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo, jijini Dar es salaam. Hivi sasa shindano hilo linawashindanisha wanafunzi wote wa shule za msingi hapa nchini.
Alisema baada ya mshindi kupatikana mwaka jana ambaye alitoka katika shule hiyo, taasisi ilibaki na changamoto ya kuwezesha kupatikana kwa maktaba, na anapoifungua maktaba hiyo anafurahishwa kuwa taasisi imetekeleza ahadi yake kwa mshindi wa shindano hilo.
Jacqueline Mengi akizungumza katika makabidhiano hayo alisema kwamba nia kubwa wa shindano hilo ni kusaidia watoto kujua kusoma na kuandika na pia kuwa wabunifu na kutumia ubunifu wao kusonga mbele.
Alisema pamoja na serikali kuwezesha elimu bure, wao kama taasisi wanatoa mchango wao ambao utasaidia kuimarishwa kwa tabia ya kusoma na kujipatia maarifa kutoka katika maktaba.
Alisema taasisi ya Dk Ntuyabaliwe iliyoanzishwa kwa ajili ya kumuenzi baba yake ambaye alikuwa anapenda sana kujisomea vitabu na kuwahimiza watoto wake akiwemo yeye kujifunza kusoma, kwa sasa inaendesha shindano hilo la Andika Challenge ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanajijenga katika ubunifu na matumizi wa lugha ya Kiswahili kwa kutunga hadithi zao wenyewe.
Anasema kwa msimu huu mashindano hayo yanaendelea na kwamba vigezo vinavyostahili kufanywa na wanafunzi kuanzia darasa la 4 hadi la 7.
Ikiamini kwamba kusoma na kuandika ndio njia pekee ya kukabiliana na wanafunzi wanaomaliza shule bila kujua kuandika Jacquline alisema kwa sasa wamewezesha shule 7 kuwa na maktaba, wanafunzi 4,406 kusaidia mambo mbalimbali na vitabu takaribani 20,827 kuwafikia wanafunzi.
Mapema Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa alisema kitendo cha kukabidhi maktaba kwa shule hiyo, Taasisi ya Dk Mtuyabaliwe imekuwa ikiunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais John Magufuli za kuboresha elimu nchini.
Wakitoa shukrani kwa niaba ya shule, Mwalimu Mkuu Doris Msigalo na Mwakilishi wa Wazazi Sudi Makamba wameishukuru Taasisi na kusisitiza kuwa wataitumia na kuitunza vizuri maktaba hiyo.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi
akisalimiana na Mwakilishi wa Wazazi na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa,
Sudi Makamba mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Shule ya Msingi
Tandale Magharibi kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba mwishoni mwa
juma jijini Dar es Salaam.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akisaini
kitabu cha wageni katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Tandale Magharibi mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio
la kuzindua maktaba lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es
Salaam.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akiuliza
maswali kwa wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi mara baada ya
kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba
lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akiimba
pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi mara baada ya
kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba
lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi
akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi mara baada
ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba
lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akikata
utepe kufungua maktaba mpya ya shule ya msingi Tandale Magharibi
iliyojengwa na taasisi hiyo jijini Dar es Salaam katika hafla
iliyofanyika mwishoni mwa juma. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Doris Msigalo (katikati), Mwakilishi wa Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa (wa kwanza kulia) pamoja na
baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akikata
utepe kufungua maktaba mpya ya shule ya msingi Tandale Magharibi
iliyojengwa na taasisi hiyo katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa juma. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa, Mwakilishi wa
Wazazi Sudi Makamba, viongozi wa bodi ya shule pamoja na baadhi ya
wanafunzi wa shule hiyo.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi na
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa
wakipitia baadhi ya vitabu vilivyotolewa na taasisi hiyo kwa ajili ya
wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi kujisomea na kuongeza
maarifa.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi
akimkabidhi moja ya kitabu mwanafunzi Nuurat Venance aliyeshinda
shindano la kutunga hadithi “Andika Challenge” lililowashindanisha
wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo, jijini
Dar es salaam na kupelekea shule yake kujengewa maktaba na taasisi hiyo.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akipewa
mkono wa pongezi na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni
Grace Mtesigwa mara baada ya kuonyesha picha za muonekano wa jengo la
maktaba ya shule ya msingi Tandale Magharibi lilivyokuwa awali.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi
akimkumbatia mwanafunzi Nuurat Venance aliyeshinda shindano la kutunga
hadithi “Andika Challenge” lililowashindanisha wanafunzi wa shule za
msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo, jijini Dar es salaam na
kupelekea shule yake kujengewa maktaba na taasisi hiyo.
Mwalimu
Mkuu wa shule ya msingi Tandale Magharibi, Doris Msigalo akitoa neno la
shukrani Muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline
Mengi mara baada ya kuwakabidhi jengo jipya la maktaba shuleni hapo.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi katika
picha ya pamoja na uongozi wa Shule ya msingi Tandale Magharibi na
baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kufungua maktaba mpya
iliyojengwa na taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi
akisalimiana na Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi.
Sandrah aliyemwakilisha mtoto wake aliyesoma shule ya msingi Tandale
Magharibi kushiriki halfa ya uzinduzi wa maktaba mpya shuleni
hapo.Katikati ni Dj wa Diamond Platnumz Romy Jones.
Muasisi
na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi katika
picha ya pamoja na Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz,
Bi. Sandrah (wa pili kulia), Dj wa Diamond Platnumz Romy Jones (wa pili
kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace
Mtesigwa (kulia) pamoja na dada wa Diamond Patnumz, Esma Platnumz.
Baadhi
ya walimu wa Shule ya Msingi Tandale Magharibi wakipiga ‘Selfie’ na
Muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi
mara baada ya kufungua maktaba mpya shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment