HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 12 January 2019

PICHA: GWARIDE LA MAADHIMISHO YA MIAKA 55 YA MAPINDUZI LEO

 KIKOSI cha Bendera cha JWTZ kikipita mbele ya Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakitowa heshima kwa mwendo wa Pole wakati wa bwaeride la kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba leo.
 GADI ya kwanza ya Gwaride rasmin la kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakipita kwa mwendo wa Pole mbele ya jukwaa la Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.
 KIKOSI cha JWTZ Wanawake wakitowa heshima kwa mwendo wa polepole wakitowa heshima mbele ya Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.
 KIKOSI cha Askari wa FFU wakipita kwa mwendo wa pole mbele ya mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Dk. Ali Mohamed Shein.
  KIKOSI cha Jeshi la Polisi Wanawake wakitowa heshima wakati wakipita jukwaa kuu Uwanja wa Gombani Pemba.
 ASKARI wa Kikosi cha KMKM Wanawake wakitowa heshima wakati wakipita Jukwaa Kuu Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba wakati wa gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 ASKARI wa Kikosi cha KMKM wakitowa heshima wakiwa katika mwendo wa kasi wakati wa maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika Uwanja wa Gombani Pemba.
 ASKARI wa Chuo cha Mafunzo wakipita kwa mwendo wa kasi wakitowa heshima jukwaa kuu, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
ASKARI wa Kikosi cha JKU wakitowa heshima kwa mwendo wa Kasi mbele ya Mgeni Tasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad