HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 15, 2019

MTOTO WA TEMBO WA ALIYETUMBUKIA SHIMONI AOKOLEWA PORI LA AKIBA LWAFI

Mamlaka ya Usimamizi wanyamapori Tanzania, inapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa mnamo tarehe 11/01/2019 majira ya saa kumi kamili jioni (10:00) Ungozi wa Pori la Akiba Lwafi Mkoani Katavi walipokea taarifa kutoka kwa Bw.Salum Summy ambaye ni  mmiliki wa shamba la Msipazi linalopakana na pori hilo kuhusu kunasa kwa mtoto wa tembo kwenye tope  aliyetumbukia ndani ya chimo eneo la china ndani ya pori hilo.

Bw. Salum alipata taarifa hizo kutoka kwa wafanyakazi wake waliyokuwa jirani baada ya kusikia tembo wakipiga kelele kwa sauti zaidi ya saa moja, na baada ya kufuatilia wakaona kundi kubwa la tembo wakijitahidi kumtoa mtoto wao kwenye shimo. Kwa vile tembo walikuwa wengi watu hao hawakuweza kuwasogelea, hivyo waliamua kuwasiliana na uongozi wa Pori la Lwafi kuhusu tukio hilo . Waliwasiliana na  Mkuu wa Kanda ya Lwafi Bw. Asubuhi T. Kasunga,na kumueleza taarifa hiyo, Bw. Asubuhi bila kuchelewa aliondoka akiongozana na askari  4 wakiwa na siraha na mahema kuelekea eneo la tukio, walifika majira ya saa 5:00 usiku na kupata taarifa ya awali toka kwa mashuhuda  wa tukio hilo,

 Kwa vile ilikuwa usiku sana  na kuhofia kuwepo kwa tembo wengine jirani  walisubiri hadi kupambazuke hadi tarehe 12/1/2019 majira ya saa 12:00 asubuhi walifuatana na wafanyakazi wa shamba pamoja na  wanakijiji jumla walikuwa 11 walifika  eneo la tukio na kumkuta mtoto wa tembo mwenye umri chini ya wa mwaka mmoja  akiangaika kutoka shimoni. Jitihada za kumuokoa zilifanyika baada ya kupanga mawe ndani ya shimo bila kumdhuru mtoto,na hatimaye walimtoa mtoto.

Baada ya kumtoa walimpelea hadi kambi ya Shamba la Msipazi. Waliwahoji wafanyakazi kujua  tembo wanaonekana muda gani kusudi waweze kumrudisha mtoto kwenye kundi, walidai kawaida wanapita majira ya saa nne usiku walisubiri siku nzima hadi muda huo lakini  hawakuonekana.  Tembo hao.

Muda wote  walikuwa wakiwasiliana na Dakitari wa tiba za wanyamapori toka Shirika la Uhifadhi liitwalo (Wildlife Conservation Society-WCS) Bi. Elizabert Stigmaier  kutoa ushauri wa chakula cha kumlisha mtoto huyo maana alionekana amechoka. Wakaelezwa wampatie Glucose aina ya DNS na aliwaeleza jinsi ya kumpa ilia pate nguvu.

Tarehe 13/1/2019  Ofisi yangu iliwasiliana na wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa wanyamapori (TAWIRI ). Idara ya wanyamapori,na WCS na kufikia uamuzi wa  tumsafirishe kwa ndege ya kampuni ya Northen Air Transport No. 5G-DEB  ambayo ilitolewa na Rusell Hastings wa Shirika la Uhifadhi liitwalo ‘ Freidkin Conservation’ hadi Arusha majira ya saa 10: 00 jioni na kupelekwa kwenye kituo cha kupokea Wanyamapori yatima kiitwacho ‘ Makoa farm Vertinary Clinic’ iliyopo Machame Wilaya ya Hai.Mtoto huyo wa tembo anaendelea vizuri.

LIMETOLEWA NA

Dkt. JAMES WAKIBARA  (KAMISHNA MHIFADHI-TAWA)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad