HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 18 January 2019

MRADI WA MAJI WA BILIONI 4.9 WAENDELEA KUHUJUMIWA NAMTUMBO

Na Yeremias   Ngerangera, Namtumbo.
Mradi wa  maji katika kijiji cha Likuyusekamaganga  wilaya  ya Namtumbo mkoani Ruvuma  umeingia   dosari tena  na kumfanya  mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia  kizigo  kuendesha zoezi la kupiga kura za siri ili kumbaini  wanaohujumu  mradi huo  baada ya  hivi karibuni  vifaa vyenye thamani  ya shilingi  milioni 500  kuteketezwa  kwa  moto  na  tukio hilo kurudia tena  siku ya  jumatatano  wiki hii na kuchoma mabomba  ya mradi huo

Mwakilishi wa kampuni  ya Elegance Developers Company Ltd  ya Dar  es salaam inayojenga mradi huo  Mhandisi  Felician Kavishe  alisema vifaa  vyenye thamani  ya shilingi milioni 500 vilichomwa  moto    na watu  wasiojulikana  hivi karibuni lakini tukio hilo hilo  limejirudia  tena kwa kuchoma  mabomba  ya kusambazia  maji ambayo  thamani  yake bado haijajulikana.

Aidha kavishe alionesha  wasiwasi  wake kwa  wafanyakazi  wa kampuni  hiyo kuendelea kutekeleza  mradi huo  katika  mazingira  ya  hofu  zilizojaa mioyoni mwao juu ya matukio  ya mara kwa mara  ya kuchoma  vifaa  na mwisho  wa  yote akadai isije  wakachomwa  na wafanyakazi  wa kampuni hiyo.

Kaimu Mtendaji wa kata ya Likuyuseka Petro Nyoni  alidai kitendo  cha mkuu wa wilaya hiyo kuendesha  zoezi la kupiga  kura za siri kwa wananchi wa kijiji  hicho  linaweza  kuwa suluhisho  la kumalizika  kwa tatizo hilo kutokana  na wananchi hao kuwajua watu wanaofanya hujuma hiyo  kwa kuwapigia kura za siri za  ushindi .

Mkuu wa wilaya hiyo aliwaambia wazee wa kijiji hicho kuwa serikali imeleta  bilioni 4.9 kutatua changamoto ya maji na kuelekeza  lawama  zake  kwa  wazee wa kijiji hicho kwa kulifumbia macho tatizo  hilo la uchomaji moto  wa vifaa vya mradi vinavyoletwa na mkandarasi huku wa zee  hao wakibaki kimya alisema mkuu wa wilaya hiyo.

“Wazee  huo ni  ujinga  kuendelea  kuacha  kudhibiti  tatizo hili ambalo mliweza kulitatua wazee wa kijiji  hiki lakini mkaendelea  kubaki  kimya na matukio  yanaendelea  kutokea  huku  wazee  wa kijiji  mpo” alisema  Mkuu wa wilaya hiyo.

Hata hivyo mkuu wa wilaya aliendesha   zoezi la kupiga kura za siri  kwa wananchi  wa kijiji hicho kuwataja  watu wanaojihusisha  na matukio  ya uchomaji moto  vifaa vya mradi huku matokeo ya kura hizo zikabaki kuwa siri kwa hatua za uchunguzi zaidi.   
 Mhandisi  mshauri Nashoni Charles  kutoka kampuni  ya Norplan  Tanzania Ltd ya Dar es salaam alisema  kitendo  cha kuendelea kuchoma  vifaa   kinaiingizia hasara  kampuni  lakini pia kitafanya  kampuni hiyo  kutumia muda mwingine kwenda kununua vifaa  , huku muda wa  mkataba wa utekelezaji wa mradi huo upo palepale.
 Kwa  mujibu wa mhandisi  mshauri wa kampuni  hiyo Nashon  alidai mradi huo  wa maji  wa Likuyumandela  umefikia  asilimia 60 kwa sasa  katika  utekelezaji wake  na unategemea kuhudumia watu 13,319 kwa kipindi cha miaka kumi baada ya kukamilika kwake.

Kaimu  Mhandisi wa maji wa Halmashauri  ya wilaya ya Namtumbo Salumu Nachundu  alidai mradi unatekelezwa chini ya progamu  ya maendeleo ya sekta ya maji (WSDP)kupitia program ndogo ya maji  na usafi wa mazingira vijijini (RWSSP)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad