HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 12 January 2019

MAKONDA:NATAMANI NIKIKUWA NIWE KAMA RAIS DK.MAGUFULI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar Salaam Paul Makonda amesema anatamani akikuwa awe Kama Rais Dk.John Magufuli. Makonda amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la upokeaji wa ndege mpya ya Airbus 220-300 ambayo imewasili nchini leo ambapo wakati anazungumza amesema anaomba viongozi wa dini wamuombee awe kama Rais Magufuli.

Amesema siku zote amekuwa akimuomba Mungu siku atakapokuwa na kuwa na umri wa utu uzima basi awe kama Rais na hivyo kuwaomba viongozi wa dini wamuombee ili ndoto yake itimie. Ametoa sababu mbalimbali za kutaka kuwa kama Dk.Magufuli ambapo kubwa ni ile ambayo amesema Rais anachokipanga ndicho anachokitekeleza,Rais ambaye hayumbushwi anapoamua kufanya maendeleo.

Makonda amesema anataka kuwa kama Rais Magufuli kwasababu ameweza kutenganisha nafasi yake ya urais na familia yake ,pia ametofautisha urais wake na urafiki."Rais Magufuli amebaki kuwa kwenye nafasi yake mwenyewe.Ingekuwa wengine leo familia ya Rais tungekuwa tunapishana nayo huko mtaani." 

Wakati huo huo Makonda amzungumzia miradi mikubwa inayoendelea nchini chini ya uongozi wa Rais Magufuli na kwamba kwenye sekta ya anga kila mwananchi ni shahidi kwa mambo yanayofanyika. Amesema idadi kubwa ya wanachi ambao wamejitokeza uwanjani hapo ni ushahidi wa kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli ambaye anatekeleza  kila ambacho amekiahidi.

"Wananchi hawa ambao wapo hapa wamekuja kwa ajili ya luunga mkono jitihada zako ambazo unazifanya kwa ajili ya Watanzania wote, tunakupongeza Rais wetu mpendwa," amesema Makonda.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad