HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 23 January 2019

LTSP YATOA MAFUNZO KWA MABARAZA YA ARDHI YA KIJIJI KUPUNGUZA MLUNDIKANO KESI ZA ARDHI ULANGA

Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kupitia mpango wake wa kuwezesha umilikishaji Ardhi(TLSP) imetoa mafunzo kwa mabaraza ya ardhi ya Vijiji 56 vilivyopo katika wilaya za Ulanga ,Kilombero na Malinyi Mkoani Morogoro ili kukabiliana na migogoro ya ardhi na namna bora ya kuisuruhisha. 

Mratibu wa mafunzo hayo James Balele amesema utafiti uliofanywa na mradi huo umebaini migogoro mingi ya ardhi imekuwa haimaliziki kutokana na uelewa mdogo wa wasuluishi,ufinyu wa vitendea kazi pamoja na miongozo ya kisheria. 

Awali akifunga mafunzo hayo ,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga, Fadhili Furaha ameishukuru wizara ya Ardhi kupitia mpango wake wa uwezeshwaji na umilikishaji Ardhi TLSP kwa kutoa mafunzo hayo yatakayo punguza migogoro kwa wananchi huku mwanasheria wa halmashauri hiyo Devota Kisembo akaeleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo mabaraza hayo ya ardhi.
Mafunzo kwa Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji katika Wilaya ya Ulanga katika kijiji cha Mavimba yakiendelea ikiwa ni sehemu ya hafla ya kuhitimisha mafunzo haya kwa wajumbe wa mabaraza wilayani humo.
Mwezeshaji kutoka Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi (LTSP) ambaye ndie mratibu wa mafunzo hayo yanayoendeshwa na LTSP akitoa salamu za utangulizi kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa Ulanga ambaye ndie alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo
Mgeni Rasmi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa Ulanga Fadhili Furaha akitoa salamu kwa washiriki wa warsha hiyo ya mafunzo.
Mmoja wa wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kijiji akichangia hoja mara baada ya mgeni rasmi kuwasili katika hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo ya mabaraza ya ardhi ya kijiji Ulanga. 
Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad