HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 16 January 2019

DOCUMENTARY KUHUSU MAONYESHO YA UTALII WA NDANI - 'UWANDAE EXPRO 2019' YAZINDULIWA DAR

Chama cha Wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na shirika la maendeleo la Ujerumani GIZ, wameandaa documentary ambayo imeziduliwa leo jijini Dar es Salaam.

Hafla ya uzinduzi wa documentary hiyo ambayo inahusu tukio la maonyesho maonesho ya Utalii wa ndani UWANDAE EXPO 2019 yatakayofanyika mwezi ujao mwezi wa Februari tarehe 15 hadi 17 katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa (National Museum –Posta). ilifanyika katika katika ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii na waandishi wa habari.

Akiongea kuhusu maonyesho haya ambayo yanafanyika nchini kwa mara ya kwanza, Mwenyekiti wa AWOTTA, ambayo inaratibu maonyesho hayo, Mary Kalikawe, alisema AWOTTA na washirika wake waamua kutekeleza mpango mkakati wa Bodi ya Utalii wa kuutangaza utalii wa ndani kwa vitendo kupitia UWANDAE EXPO 2019 na kauli mbiu ya maonyesho haya ni “Tambua ushindani wa Kibiashara katika Utalii wa Ndani Tanzania”.

“Kuzindua kwa documentary hii ikisisitiza mchango wa akina mama “Nani kama mama” kunaenda sambamba na kuzindua matangazo kwa umma wa Tanzania juu ya uwepo wa sekta kubwa ya utalii humu nchini ambayo ni muhimu ikatambuliwa kusudi ihudumiwe na kupewa umuhimu wake. Sekta hii inachochea uwekezaji kwa wingi kama tunavyoona mahoteli, usafirishaji tangu wa ndege hadi wa bodaboda, biashara ya chakula kila pembe ya nchi, burudani na utalii wa aina nyingine nyingi. Sambamba na uwekezaji huu, sekta ina uwezo mkubwa wa kutengeneza ajira kwa wakubwa na wadogo pia inabeba uwezo mkubwa wa kutengeneza kipato kwa mtu mmoja mmoja, makundi na kuchangia kipato cha taifa kwa kiasi kikubwa. Kwa sasa utalii wa mbuga za wanyama unachangia asilimia 17 ya pato zima la taifa ambayo ni takribani dola Bilioni 2.1 au shillingi zaidi ya trillion 4.7 kila mwaka”. alisema Kalikawe.
Mwenyekiti wa Chama cha wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (kushoto) akiongea na wandishi wa habari ( hawapo pichani ) jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutangaza Maonyesho ya biashara ya Utalii wa Ndani ya Kwanza nchini yatakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Posta Dar es Salaam, Februari 15 hadi 17 ,2019. ” Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni Tambua Ushindi wa Kibishara katika Utalii wa Ndani Tanzania” Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TTB ,Geofrey Tengeneza na Mwenyekiti wa chama cha wanawake Tanzania katika biashara (Tanzania Women Chamber of Commerce) Jacqueline Maleko.
Mwenyekiti wa Chama cha wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (kushoto) Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) ,Geofrey Tengeneza (katikati) na Mwenyekiti wa chama cha wanawake Tanzania katika biashara (Tanzania Women Chamber of Commerce) Jacqueline Maleko, wakiwa wameshikana mikono kuonyesha ushirikiano wao kwa wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutangaza Maonyesho ya biashara ya Utalii wa Ndani ya Kwanza nchini yatakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Posta Dar es Salaam, Februari 15 hadi 17 ,2019.” Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni Tambua Ushindi wa Kibishara katika Utalii wa Ndani Tanzania.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad