MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati akifunga Mashindano ya Kombe la Kabunda Cup |
MKUU wa wilaya ya Muheza
Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa
Mashindano ya Kabunda Cup Nahodha wa timu ya Ushirika Amiri Nko
kushoto ni Afisa Michezo wa wilaya ya Muheza Anania Sama
Nahodha wa timu ya Ushirika
Amiri Nkoa akiwa ameinua kombe hilo juu mara baada ya kukabidhiwa.
Katibu Msaidizi wa Kamati ya Mashindano hayo akisoma risala
MKUU wa wilaya ya Muheza
Mhandisi Mwanasha Tumbo katika akiwa kwenye picha ya pamoja na
wachezaji
Sehemu ya Mashabiki wa soka wakiwa wamnefuatilia mchezo huo
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mwanasha Tumbo amesema
atashirikiana na wanamichezo ili kuhakikisha wanaweza mazingira mazuri
yatakayowezesha kupatikana timu ambayo itaweza kushiriki ligi madaraja
ya juu ikiwemo Ligi kuu.
Mwanasha aliyasema hayo wakati
fainali michuano ya kombe la Kabunda Cup iliyokuwa ikichezwa kwenye
viwanja vya Vikonge Mtindiro wilayani Muheza ambapo alisema ili kuweza
kuhakikisha wanafanikisha jambo hilo wataendelea kuhamasisha vijana
kujikita kwenye michezo.
Alisema licha ya kuhamasisha
michezo kutokana na kwamba ni ajira ambayo inaweza kuwainua vijana
kuichumi na kupata maendeleo lakini pia aliwahaidi kuwajengea kiwanja
cha mpira chenye matofali ili waweze kuonyesha umahiri wao na hatimaye
wilaya hiyo iweze kupata mafanikio kwenye soka.
“Leo
nimekuja hapa kuhimitisha Ligi hii kwanza nimefurahishwa sana na
viwango ambavyo mmekuwa mkivionyesha kwenye mchezo huu nimeongeza na
Diwani wenu hapa na niwahaidi kwamba nitawajengea kiwanja chenye
matofali ili hari ya kushiriki kwenye michezo muweza kuendelea nayo na
tunaamini siku zijazo tutairudisha Muheza kwenye ramani ya soka
“Alisema DC Mwanasha.
Alisema kwamba anafanya hivyo ili
kuweza kuchochea maendeleo ya mchezo huo ambao vijana wakiweka bidii
na nia wanaweza kufika mbali ikiwemo kuitangaza wilaya hiyo lakini pia
kupata manufaa kama walivyokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu
ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Awali
akizungumza katika fainali hiyo Katibu Msaidizi wa Kamati ya
Mashindano hayo Salehe Mwinjuma alisema lengo la mashindano hayo
yalikuwa ni kuweza kuinua vipaji vya wachezaji wachanga kwenye Kata
hiyo yaliyoanzishwa na mdau wa michezo Seif Kabunda kwa kushirikisha
timu 20 zilizocheza kwa mtindo wa makundi.
Alisema kwamba
msimu ujao ligi hiyo itakuwa na mabadiliko makubwa kutokana na
mdhamini wa mashindano hayo kuamua kujipanga upya na kuja kinyengine
lengo kubwa likiwa kuhakikisha michezo inapata mafanikio.
Katika fainali hiyo timu ya Ushirika FC waliweza kuibuka na ushindi
wa mabao 2-1 na kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Kabunda Cup
baada ya kuibamiza Kwarabuye FC mabao 2-1 katika mchezo wa fainali
uliochezwa kwenye uwanja wa Vikonge Mtindiro na kujiny’akulia kombe na
kitita cha sh.milioni moja . Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali na
wenye ushindani mkubwa uliohudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza
Mwanasha Tumbo ambaye ndie alikabidhi zawadi kwa washindi kwenye
michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment