HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 7, 2018

WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKULIMA WA KOROSHO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Korosho cha Terra Cashew, Leonardo Denti  (wapili kulia) wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kazi ya ubanguaji korosho wakati alipotembelea kiwanda cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.  Wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kazi ya ubanguaji korosho wakati alipotembelea kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.  Wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama korosho zilizobanguliwa wakati alipotembelea kiwanda cha korosho cha Terra kilichopo Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo na katikati ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda, Leonardo Denti.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama korosho zilizobanguliwa wakati alipotembelea kiwanda cha korosho cha Terra kilichopo Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo na kulia ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda, Leonardo Denti.
 Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kutembelea kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018. 
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaresti Ndikilo akizungumza  kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  ili azungumze  wakati Waziri Mkuu alipotembelea kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotembelea kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.
Wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho, Desemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wananchi hususan wakulima wa korosho nchini baada ya kuwahakikishia kuwa korosho zao zote zitanunuliwa. Amesema Serikali kupitia Bodi ya Mazo Mchanganyiko itanunua korosho zote na hakuna korosho za wakulima nchini ambazo zitabaki bila ya kununuliwa.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra akiwa njiani kwenda Dodoma. Waziri Mkuu amesema bodi hiyo inaendelea kufanya thamini na kujiridhisha kama kweli korosho hizo zimezalishwa nchini na kuangalia viwango vya ubora.

Amesema baada ya kujiridhisha kuhusu viwango vya ubora na mkulima aliyepeleka ndiye mwenyewe ndipo taratibu za malipo hufanyika. Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kununua korosho baada ya wafanyabiashara kutaka kuzinunua kwa bei ya chini ambayo haikuwa na tija.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha mkulima ananufaika na ndipo Rais Dkt. John Magufuli alisitisha ununuzi baada ya kuona wakulima wanataka kudhulumiwa.” Waziri Mkuu amesema kuwa hadi sasa tayari tani 181,000 zimeshakusanywa, hivyo amewataka wakulima wa zao hilo nchini waendelee kuiamini Serikali yao.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuunga mkono jitihada za Serikali kukuza uchumi kwa kupitia sekta viwanda. Awali, Meneja Utawala wa kiwanda cha Terra, Peter Ngwale alisema uwezo wao ni kubangua tani 6,000 kwa mwaka, ambapo tayari wamebangua tano 3,000. Pia aliiomba Serikali iwasaidie katika suala la ubora wa korosho kwa kuwa kiwango cha ubora kinachoandikwa kinakuwa tofauti na uhalisia wa korosho  yenyewe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad