HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 3 December 2018

Viwanda vya dawa vinahitaji watalaam wa Kemia na Biolojia

Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi amesema viwanda vya dawa vinahitaji watalaam wenye msingi wa Masomo ya Kemia na Biolojia. Profesa Kambi ameyasema hayo leo wakati wa utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Biolojia na Kemia katika matokeo ya kidato cha Nne na Sita kwa mwaka 2018 iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda ambapo vitajengwa viwanda vya dawa hivyo kunahitajika wabobezi wa katika masomo ya Kemia na Biolojia kwa ajili ya kuendesha viwanda hivyo. Aidha amesema kuwa masomo hayo wanatakiwa wanafunzi kujituma zaidi ikiwa na wazazi kuwatia moyo wa kufanya vizuri katika masomo ya sayansi. Profesa Kambi amempongeza mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuanzisha tunzo hizo kwani inawatia moyo wanafunzi kuendelea kuvutika katika kusoma masomo ya Kemia na Biolojia.

Nae Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa wamekuwa wakitoa tunzo kwa wanafuzi kwa kuwapa cheti pamoja na Fedha. Amesema kwa huu jumla ya wanafunzi waliopata cheti na fedha ni 24 na walimu wanne wa masomo hayo. Wanafunzi hao wamepata kuanzia sh.500000 hadi 350 kwa wakwanza hadi wa tatu.  Amesema katika matokeo hayo shule za serikali ni Nne ambazo zimetoa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Biolojia kwa mwaka 2018.

Aidha amesema kuwa wataendelea kuhimiza wanafunzi katika kusoma masomo ya sayansi ambayo ni Kemia na Biolojia ili taifa liweze kupata watalaam wengi hasa katika kuhudumia viwanda mbalimbali.
 Mkurugenzi wa Biashara wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, George Kasinga akitoa maelezo ya tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Biolojia na Kemia mwaka 2018.
 Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza kuhusiana utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha Nne na Sita mwaka 2018 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Esthehellen Jason akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya kidato cha Nne na Sita iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam
 Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi akizungumza wakati wa utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya kidato cha Nne na Sita mwaka 2018 iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi akimkabidhi Cheti  Mwanafunzi aliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha Nne katika Masoko  Biolojia na Kemia Liliani Katabalo katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam.
 Mwanafunzi Biubwa Khamis Ussi akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya kidato cha Nne na Sita katika mitihani ya Biolojia na Kemia  katika hafla ya utoaji tunzo iliyofanyika katika viwanja mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam.
 Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Biolojia na Kemia kwa kidato cha Nne
Mkemia na wazazi wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Biolojia na Kemia kwa matokeo ya kidato cha Nne na Sita
 Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi akipata maelezo katika maonesho ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika hafla ya utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha Nne na Sita mwaka 2018 iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

1 comment:

  1. Hili ni jambo zuri katika kuwafanya wanafunzi kuongeza bidii na kuwapa moyo kwani hawa ni raslimali ya baadae katika kuijenga nchi yetu. Afisi ya mkemia tunawapongeza

    ReplyDelete

Post Bottom Ad