HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 19 December 2018

VIGOGO CAF WAKAGUA HOTELI, HOSPITAL KUPANGA RATIBA YA AFCON U17 KESHO

Rais wa 
 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia .

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KUELEKEA Fainali za Vijana U17 za Africa zitakazofanyika mwakani 2019 Tanzania   Upangaji wa ratiba unatarajiwa kufanyika  kesho Alhamis Disemba 20,2018 kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Dar es salaam.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema tayari wamepokea ugeni kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF ambao upo nchini kwa upangaji wa ratiba.

Ujumbe huo wa CAF ukiwa hapa nchini umetembelea na kukagua uboreshaji wa miundo mbinu ya viwanja unaoendelea.

Rais wa TFF Ndugu Karia amesema baada ya kutazama maendeleo ya Viwanja watashauri zaidi kulingana na walivyoona maendeleo hayo.

Amesema mbali na Viwanja ujumbe huo wa CAF umetembelea Hoteli na Hospitali.

Kesho watahudhuria upangaji wa ratiba ya Fainali za Vijana U17 za Afrika zitakazofanyika kuanzia saa 12 jioni na Dunia itapata kushuhudia upangaji huo moja kwa moja kwenye Televisheni.

Wajumbe wa CAF waliopo nchini ni Samson Adamu,Yasmin Hossam Eldin El Ehwany,Amri Ali Sadek,Mohamed Bakeer,Fayrouz Mahml,Mohamed Alaa El Shizy,Dina Medat,Moses Magogo anayewakilisha Kamati y Utendaji ya CAF wakati Leodger Tenga Mjumbe wa Kamati ya Utendaji CAF atakua mwenyeji wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad