HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 10 December 2018

UONGOZI WA PRECISION AIR WAOMBA RADHI ABIRIA NDEGE ATR 72 KUPATA HITILAFU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

SHIRIKA la Ndege la Precision Air wameomba radhi abiria wao baada ya ndege yao ATR 72 kupata hitilafu ya kushambuliwa na ndege wakubwa  na kushindwa kuendelea na safari.

Uongozi wa Precision Air umethibitisha kuwa ndege yao PW 722 itokayo Nairobi kupitia Kilimanjaro hadi Mwanza ilipa hitilafu na kushindwa kuendelea na safari.

Wakitoa taarifa hiyo uongozi wa Precision Air amesema kuwa ndege hiyo PW 722 ilipata hitilafu ila ilifanikiwa kutua katika Uwanja wa ndege wa Jijini Mwanza.

Wamesema kutokana na uwezo na ujuzi walionao marubani pamoja na wahandisi waliweza kufanikisha kutua salama.

Ndege hiyo ilitua salama kabisa na kuhusu timu ya wahandisi wameendelea  na kurekebisha thanzo cha tatizo na wameahidi abiria wote watafika sehemu wanazoenda salama.

Aidha, abiria wote waliothirika wameshauriwa kubadilisha ndehe na wameombwa radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na timu yao inaendelea kulifanyia kazi hilo ili kuweka ratiba sawa.Shirika la ndege la Precision Air daima litaendelea kuhakikisha usalama wa abiria na mamlaka husika itahakikisha kuwa matukio kama hayo hayajitokezi tena.

Ndege ilipata hitilafu hiyo baada ya kuvamiwa na kundi la ndege wakubwa, ndege hiyo aina ya PW 722 ilibeba abiria 68 na wahudumu wanne.
Ndege aina ya ART 72 ilipotua salama kwenye Uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kushambuliwa na ndege wakubwa.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad