Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akimkaribisha aliyekuwa Balozi Tanzania nchini Zimbabwe Lt. Gen.Mstaafu Charles Makakala mara alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Dar es Salaam leo Desemba 05, 2018 kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa Jeshi hilo na kufanya mazungumzo na uongozi wa Jeshi la Magereza.
Aliyekuwa Balozi Tanzania nchini Zimbabwe Lt. Gen.Mstaafu Charles Makakala (wa pili kulia) akifafanua jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza leo Desemba 05, 2018 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Dar es Salaam.
Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Zimbabwe Lt. Gen.Mstaafu Charles Makakala akisalimiana na Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Nicas Banzi (2002-2007) walipokutana Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Dar es salaam leo Desemba 05, 2018.
Lt. Gen.Mstaafu Charles Makakala aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza leo Makao Makuu ya Jeshi hilo. Watatu kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike. Kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama na Kamishna wa Miundombinu ya Magereza na Uzalishaji, Tusekile Mwaisabila. Kushoto ni Kamishna wa Fedha na Mipango, Gedion Nkana na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Augustino Mboje. (Picha zote na Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment