HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 5, 2018

TGNP WAADHIMISHA NA KUJADILI SIKU 16 ZA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KATIKA kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wamefungua kongamano la kampeni ya siku 16 za kupambana na ukatili wa kijinsia. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano hilo Mkurugenzi mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi amesema kuwa Wanawake ni nguvu kazi ya Taifa na pasipo kumthamini hakutokuwa  na Maendeleo ambayo yatakua na usawa wa kijinsia na haki sawa.

Amesema kuwa kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa mwanamke ni usalama wake na ni jukumu la kila mmoja katika kutokomeza ukatili wa kijinsia na hasa kuwalinda wanawake katika janga hilo. Kuhusiana na  rushwa ya ngono makazini hasa kwa waajiri kwenda kwa waajiriwa bi. Lilian amesema kuwa kupitia kampeni hiyo hali hiyo itavunjwa na kupigwa vita kwani elimu itatolewa kwa pande zote ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa na uhuru na ujasiri wa kusema pindi anapokutana na changamoto hizo.

Aidha amesema kuwa wao kama TNGP mtandao wataendelea kuunga mkono juhudi zote zitakazofanywa na na TAKUKURU na vyombo vingine vya dola katika kuhakikisha vita hiyo inafanikiwa na ametoa wito kwa serikali na wadau wengine kushirikiana katika kuhakikisha janga hilo la ukatili linatokomea kabisa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya wanawake (TUCTA) Rehema Ludanga amesema wanaunga mkono siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa lengo la kukomesha kama si kuondoa kabisa dhana ya ukatili hususani Kwenye  maeneo ya kazi.

 Ludanga amesema kuwa ukatili wa kijinsia pia unahusisha  rushwa ya ngono mahali pa kazi na kwa kiasi kikubwa ipo katika  sekta binafsi na hiyo husababishwa na  waajiriwa kutofikia vigezo vya kuajiriwa hivyo inawalazimu kutoa  rushwa  ya ngono ili waweze kupatiwa nafasi za kazi kwa haraka .

Vilevile amefafanua Changamoto zinazowakumba watu  wanaofanyiwa ukatili huo hasa wanawake ni kuwepo kwa usiri pamoja na hali ya kutojua kujieleza au kufikisha taarifa Kwenye vyombo husika ikiwemo  dawati la kijinsia na ustawi wa jamii ambao wanahusika na kutatua matatizo hayo.

 Amesema kuwa wataendelea kupiga vita dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake pamoja na watoto ili kuwepo kwa  haki sawa bila kujali jinsia moja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo ameeleza kuwa wapo bega kwa bega na serikali pamoja na vyombo vya dola katika kuhakikisha janga hilo linatokomea kabisa wakati wa kongamono hilo lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao  leo jijini Dar es Salaam.
Wadau pamoja na wadua mbalimbali kutoka vitovu vya jinsia  na Clabu za jinsia Mashuleni wakiwa kwenye kongamono la kupinga ukatili wa kijinsia lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao  leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa kamati ya wanawake (TUCTA) Rehema Ludanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kugmfunguliwa kwa kongamano hilo ambapo amesema kuwa taasisi binafsi zinaongoza kwa rushwa ya ngono mahali pa kazi wakati wa kongamono hilo lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao  leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad