HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 5 December 2018

TAEC YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI NAMNA YA KUTATUA CHANGAMOTO MADHARA YA MIONZI

Na Vero Ignatus,Arusha
Tume ya nguvu za ATOMIC Tanzania kwa kushirikiana na jumuiya ya umoja wa Ulaya EU imeandaa warsha ya siku 3 kwa ajili ya utowaji wa leseni ya madini yatoayo mionzi ya kujikinga na madhara yake nchini Tanzania

Warsha hiyo iliyofanyika jijini Arusha katika Ofisi za Atomic zilizopo Njiro ambapo lengo ni kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta mbalimbali ili kuweza kutatua changamoto zinazotokana na madhara ya mionzi

Mkurugenzi wa tume ya nguvu za Atomic Tanzania Prf. Lazaro Lusagara amesema kuwa wameendelea na warsha hiyo ili kuweza kuhakikisha wanaziba mianya ambayo imekuwa wazi na kuweza kuwafikia watanzania wote kwa wakati ili kuweza kuwapa elimu ya kutosha

Mkurugenzi wa lessen za madini pamoja na mifumo ya TEHAMA nchini Tanzania Bw. Thomas Ngole Pamoja Khadija ramadhani kutoka tume ya madini Tanzania wamesema semna hiyo itasaidia kuongeza nguvu katika utendaji kazi na kusaidia Radio active Material kuwaweka watu salama

Kwa upande wake Afisa mazingira kutoka baraza la taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira Bw. Abel Nestori Sembeka amesema kuwa semina hiyo itasaidia kuboresha namna ya utendaji kazi ili kuweza kujua shughuli za kusimamia madini ya URANIUM na utendaji wa kazi mzuri na kufanya kazi kwa ushirikiano

Hata hivyo wadau mbalimbali walioshiriki ni pamoja na, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, wizara ya maliasili na utalii, baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC, tume ya madini, tume ya nguvu za Atomic Tanzania, na wizara ya elimu sayansi na Technologia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad