HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 20 December 2018

SIMBA WAPASHA KIPORO CHA KMC, WATOKA NA USHINDI WA 2-1

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Timu ya Simba imefanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Kinondoni Municipal Council (KMC) mechi iliyochezewa katika dimba la Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ulioanza kwa kasi ilichukua dakika 11 ya kupitia kwa mshambuliaji Adam Salamba kuiandikia vijana wa Msimbazi goli la kuongoza.

Simba waliendelea kulisakama lango la wapinzani wao na baada ya dakika tatu ikiwa ni  dakika ya 14, Said Ndemla anaiandikia goli la pili kwa shuti kali nje ya kumi na nane na kuzidi kudidimiza matumaini ya KMC kuondoka na ushindi kwenye mchezo.

Mpaka mapumziko, Simba walienda kifua mbele wakiwa wanaongoza kwa goli 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Kocha wa KMC akifanya marekebisho kwa kuwatoa wachezaji wawili na kuingiza nguvu mpya.

Mpira ulikuwa wa kasi na kila mmoja akisaka goli na katika dakika ya 67,  KMC walifanikiwa kupata goli kupitia kwa mchezaji wake James Msuva na kupelekea matokeo yake kuwa 2-1.

Mpaka kipengya cha mwisho kinapulizwa Simba wanaibuka kidedea kwa  ushindi wa goli 2-1 na kufikisha alama 30 akisalia kwenye nafasi ya tatu akiwa nyuma ya Yanga mwenye alama 44 na Azam 40.

Kikosi cha Simba kimeweza kumuanzisha mchezaji wake mpya Koulbaly pamoja Haruna Niyonzima, Asante Kwasi na Jurko Murshid waliokosekana kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad