Serikali imewaagiza viongozi wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kata ya Parakuyo kuhakikisha wanawaondoa wavamizi waliovamia Ranchi ya Narco Mkata. Agizo ilo limetolewa na Naibu waziri wa mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati alipokuwa anafanya ziara wilaya Kilosa kwa lengo la kusikiliza kero za wafugaji. "Msimuonee mtu ambae analima nje Ranchi NARCO na hakikisheni mnawapokonya vitalu waliopewa wakashindwa kuviendeleza ili wapewe wafungaji wengine alisema Ulega"
Mhe Ulega aliwaeleza wafugaji maagizo yake kwa viongozi wa wilaya juu ya kuwaondoa wavamizi katika Ranchi ya NARCO Mkata na wote wanaolima katika maeneo hayo na wakodishiwe wafugaji kwa ajili ya kunenepesha Mifugo yao katika vitalu vitakavyokuwa vimeandaliwa. Alisema Wilaya inakuja na majina ya wafugaji na idadi ya mifugo yao wanaohitaji vitalu hivyo.
"Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na Rais wetu anawapenda sana wafugaji na watu wote anatupenda na alishatupa maagizo kama wizara kuwaondoa watu waliohodhi maeneo ya Ranchi na kuwapa wafugaji wetu"
Wakati Mhe. Ulega akijibu hoja ya wafugaji kukosa elimu ya ufugaji wa kisasa wenye tija ikiambatana na elimu ya uzalishaji wa malisho aliwaagiza wataalam wa mifugo kutoka Wakala wa Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Mifugo (LITA) alioongozana nao katika ziara hiyo kupeleka wanafunzi kujifunza kwa vitendo katika kata ya Parakuyo na maeneo mengine ya wafugaji ili waweze kusambaza elimu hizo kwa wafugaji kuliko wanafunzi hao kufanya mafunzo hayo maeneo ya mijini.
Naye Mkuu wa wilaya Kilosa,Adam Mgoi Ametoa wito kwa wafugaji wote wilayani kilosa kuwa wa kweli pindi wanapohiyajika kuorodhesha mifugo yao,ili kuweza kuweka mipango mizuri ya kuwasaidia.Aidha wafugaji walimpongeza na kumashukuru sana Mhe Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwajali na kuwatetea wanyonge pia kwa mradi wa reli ya Standard gauge ambao umewapa ajira vijana wao na pia utasaidia katika usafirishaji wa mifugo yao kwenda kwenda Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wafungaji katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Parakuyo wilaya Kolosa mkoa wa Morogoro ambapo amewahakikishi kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu,majosho mabirika ya maji.
Baadhi ya wafungaji wa wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega.
Meneja wa Rachi ya Mkata wilaya ya Kilosa, Sadalah Athuman(kulia) akitoa taarifa fupi ya mikakati waliyoiweka kuwasaidia wafungaji wa wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega
No comments:
Post a Comment