NA LUSUNGU HELELA-MWANZA
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu amewataka wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani ya Hifadhi ya misitu ya Visiwa vya Kome na Maisome vilivyoko wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kulipa tozo za serikali bila kulazimishwa.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Shigala ulioko Kome Mchangani ambayo ni kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dkt. Charles Tizeba amemueleza Naibu Waziri hiyo kuwa kumekuwepo na changamoto ya ulipaji tozo kubwa hata kama mtu ana eneo dogo na ndipo wananchi walilazimika kugoma kulipa tozo hiyo kwa lengo la kupata msaada zaidi.
Amefafanua kuwa mtu anayemiliki hekari moja anatakiwa kulipa Tsh.425,000 kwa mwaka lakini hata mtu anayemikili eneo dogo la mita 20 naye anatakiwa kulipa kama wa hekari moja kitendo kilichowafanya wananchi hao kushindwa kulipa na kusubili maelekezo ya wizara husika.
Mmoja wa wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi hiyo,Juma Ramadhani amemwomba Naibu Waziri kuangalia upya sheria hiyo ili wananchi wapate nafuu ya kulipa na serikali iweze kupata mapato yake.
Kaimu Meneja wa TFS Kanda ya Ziwa, Thomas Moshi amesema kuwa tozo hizo zipo kwa mujibu wa sheria kinachotakiwa ni wananchi kulipa na siyo kugomea kulipa tozo hizo na wanapofanya hivyo wanakwenda kinyume na matakwa ya sheria ya hifadhi ya misitu.
Kanyasu amewahakikishia wananchi hao kuwa suala hilo atalipatia majibu kwa haraka lakini amewataka watu wanaomiliki hekari moja kulipa tozo hizo kwa wakati na wale wenye maeneo madogo madogo wajiunge katika vikundi ili waweze kuilipa pesa hiyo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kuwa watalipa tozo za serikali bila kulazimishwa alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Dkt. Charles Tizeba akizungumza na wananchi wa Jimboni kwake kwenye mkutano wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu wa kutatua kero za wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya katika kijiji cha Kisaba na Bugombe.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Buhama kata ya Buhama, Thomas Sabuni, akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kabala ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ikiwa lengo kutatua kero za wananchi wa Kisiwa hicho wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya katika eneo la Kome mchangani.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu akiteta jambo na Meneja wa Shamba la Buhindi , Ayoub Kigongwira wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu ndani ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Buhama wakati alipowasili katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wvuvi kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiiangalia taarifa mara baada ya kukabidhiwa taarifa Mwenyekiti wa kijiji Buhama, Thomas Sabuni wakati alipowasili katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wvuvi kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)
No comments:
Post a Comment