HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 6, 2018

Mwenyekiti Chadema kuendelea kusota rumande hadi Desemba 21

Na Karama Kenyunko blogu ya Jamii.
Kesi ya uchochezi dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko  na wenzao saba inayounguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepigwa kalenda hadi Desemba 21 mwaka huu.

Aidha mahakama hiyo imetoa ruhusa kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuendelea kuhudhuria michezo ya Afrika Mashariki nchini Burundi na pia imeruhusu Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, kumuuguza mkewe ambaye amejifungua kwa upasuaji hivi karibuni.

Mbowe na Matiko wataendelea kukaa mahabusu kwa muda usiojulikana pengine hadi mwakani,  baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusimamisha usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na washitakiwa hao kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu ya kuwafutia dhamana.

Hatua hiyo imetokana na upande wa serikali kukata rufaa kupinga maamuzi ya Jaji Sam Rumanyika aliyesema kuwa rufaa ya kina Mbowe ipo mahakamani hapo kisheria na kwa maana hiyo, haina mamlaka ya kuendelea na usikilizwaji wa rufaa hiyo.

Akitoa maamuzi hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, Jaji Rumanyika alisema. DPP anapewa mamlaka ya kukata rufaa kwa uamuzi mdogo ambao haumalizi kesi chini ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa na kwamba kunapokuwepo taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani, mahakama ya chini haiwezi kuendelea na shauri.

Mapema leo,Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amedai mbele ya Hakimu Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba washitakiwa Mdee na Heche hawapo mahakamani.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala amedai kuwa Heche alitolewa taarifa kuhusu kufanyiwa upasuaji mdogo kwa mke wake lakini afya ya mtoto sio nzuri sana na kwa upande wa Mdee yupo nchini Burundi kushiriki mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki.

Mdhamini wa Mdee, Fares Robinson aliieleza mahakama hiyo kuwa Mdee yupo safarini kwenda Burundi kwa safari za kibunge na kwamba Katibu wa Bunge aliandika barua kwa Hakimu Mfawidhi wa mahakama kumtaarifu kuwa mshitakiwa huyo atakuwa nje kwa shughuli za kibunge na kwamba atarudi Desemba 20, mwaka huu.

Akijibu hoja hiyo, Wakili Nchimbi alidai walipokea hati ya wito ikiambatanishwa na maombi ya ruhusa ya kupitia Mdee kupitia kwa Katibu wa Bunge.

Alidai kwa mantiki hiyo wanaona washitakiwa wanafuata taratibu na hawana pingamizi na hilo na kuhusu Heche anayemuuguza mkewe pia hawana pingamizi ikizingatiwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mashauri alisema kuwa walipokea barua kutoka kwa Katibu wa Bunge kuomba ruhusa ya Mdee kwenda Burundi kuhudhuria michezo ya EAC na kwamba pande zote za utetezi na mashitaka walikuwa Mahakama Kuu kwa kesi nyingine.

"Mahakama inamruhusu mshitakiwa kuhudhuria michezo na ruhusa ya Heche ya kumuuguza mkewe imekubaliwa lakini wazingatie kuwepo mahakamani siku ya kutajwa kesi hiyo Desemba 21, mwaka huu, " alisema Hakimu Mashauri.

Muda wrote wakati kesi hiyo inaendelea  mahakamani hapo kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi ambapo uliwazuia baadhi ya wafuasi wa chama hicho kuingia mahakamani na badala yake waliwaruhusu viongozi wa chama hicho  pekee.

Washitakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya  na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu  

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

Mwisho
[02:54, 12/6/2018] Karama: Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeiahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, mdogo wa mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz, Akram Aziz, kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Akram ambaye alifikishwa mahakamani hapo Oktoba 31, 2018 na kufunguliwa keai namba 82/2018 anakabiliwa na mashitaka 75 yaikiwemo ya kukutwa na nyara za serikali, silaha, risasi na utakatishaji fedha wa dola za Marekani 9,018.

Wakili wa Serikali, Mkunde Mshanga  amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizile, kuwa kesi hiyo leo Desemba 6.2018 imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado haujakamilika.

Kufuatia taarifafa hiyo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 13, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Akram  anakabiliwa na mashitaka mawili ya kukutwa na nyara za serikali, mashitaka 70 ya kukutwa na silaha, mashitaka mawili ya kukutwa na risasi zaidi ya 6,496 na moja la utakatishaji fedha.

Inadaiwa  kuwa Oktoba 30, mwaka huu mshitakiwa akiwa maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, alikutwa na nyara za serikali ambayo ni meno sita ya tembo yenye thamani ya dola za Marekani 45,000 sawa na Sh 103, 095,000, mali ya serikali.

Pia inadaiwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni, mkoani humo Akram alikutwa na nyara za serikali ambazo ni nyama ya nyati yenye uzito wa kilogramu 65, yenye thamani ya dola za Marekani 1,900 sawa na Sh 4,352,900 mali ya serikali bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapoli nchini.

Katika mashitaka ya tatu hadi la 72, kwamba siku hiyo na eneo hilo hilo, mshitakiwa huyo alikutwa na silaha aina ya Pistol bila ya kibali cha mrajisi wa silaha.

Inadaiwa katika mashitaka ya 73 kuwa, Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay mshitakiwa alikutwa na risasi 4,092 na katika mashitaka mengine ilidaiwa mshitakiwa alikutwa na risasi 2,404 bila kuwa na kibali.

Katika mashitaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo hayo ya Oysterbay, Akram alitakatisha USD 9,018 huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kujihusisha na makosa ya uhalifu. 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzake leo Mahakamani Kisutu.
viongozi mbalimbali wa Chadema wakiwa mahakamani Kisutu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad