HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 18, 2018

MultiChoice yafunga mwaka na waandishi Msasani Beach Club

Kampuni ya MultiChoice Tanzania, imefanya sherehe ya kufunga mwaka na kuwashukuru waandishi wa habari kwa ushirikiano wa kikazi waliokuwa nao katika kipindi cha mwaka huu wa 2018.
Sherehe hiyo ya kuwashukuru waandishi  ilifanyika Msasani Beach Club iliyopo katika fukwe za bahari ya Hindi, Kawe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa sherehe hiyo na waandishi, Meneja Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria alisema ‘Tunayofuraha kubwa kujumuika pamoja na waandishi kutoka vyombo mbali mbali ambavyo kampuni yetu ya Multichoice imekuwa ikishirikiana nanyi katika kipindi cha mwaka huu wa 2018. Tunapenda kutoa shukrani zetu dhati na zaidi kutegemea ushirikiano wenu katika kipindi cha mwaka ujao”.  

Sherehe hiyo ya kufunga mwaka na waandishi pia ilienda sambamba na mtanange mkali baina ya timu ya mpira wa miguu ya wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania na timu ya chama cha waandishi wa habari za michezo maarufu kama TASWA FC ambapo waandishi hao waliweza kuibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 2 -1 dhidi ya MultiChoice. 
 Baadhi ya waandishi na wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiburudika kwa vinywaji katika sherehe ya Media Day iliyofanyika Msasani Beach Club mwishoni mwa wiki.
 Meneja Masoko Alfa Mria akizungumza katika hafla hiyo wakati akitangaza zawadi.
 Meneja Uajiri wa Multichoice Tanzania Tike Mwakitwange akimvisha nishani kapteni wa timu ya TASWA FC Bw. Majuto Omary mara baada ya mchezo wa timu hiyo na DSTV FC kwenye hafla ya Dstv Media Day iliyofanyika kwenye ufukwe wa Msasani Beach Club Kawe jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Meneja wa Fedha Multichoice Tanzania Bw. Godfrey Bwana akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku katika hafla ya Dstv Media Day iliyofanyika mwishoni mwa wiki Msasani Beach Club Kawe jijini Dar es salaam.
 Meneja Msoko Alfa Mria aliyekuwa refa wa mchezo kati ya DStv na TASWA akitoa kadi ya njano kwa mmoja wa wachezaji wa timu ya TASWA FC baada ya kucheza vibaya.

 Baadhi ya waandishi na wafanyakazi wa MultiChoice wakiserebuka katika sherehe ya Media Day mwishoni mwa wiki. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad