HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 19 December 2018

MOHAMED ISSA 'BANKA' ARUHUSIWA KUANZA MAZOEZI BINAFSINa Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mchezaji Mohamed Issa 'Banka' ameruhusiwa kuanza mazoezi wakati akikaribia mwisho wa adhabu yake ya kufungiwa baada ya kubainika kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya bangi.

Banka baada kubainika kutumia dawa hizo alifungiwa kwa kipindi cha miezi 14 kuanzia Disemba 9,2017 na adhabu kumalizika Februari 8,2019.

Pamoja na kuruhusiwa kuanza mazoezi Banka  kucheza mchezo wowote ule zaidi ya kufanya mazoezi.

Mchezaji huyo alifungiwa na Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni ya Kanda ya Tano Africa (RADO).


Banka alisajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili katika dirisha la usajili la mwezi June akitokea timu ya Mtibwa Sugar lakini hakuweza kushiriki kwenye mchezo wowote kutokana na kufungiwa kutokushiriki masuala ya kimichezo ikiwemo kufanya mazoezi sehemu atakayoonekana na watu.

Adhabu yake inatarajiwa kumalizika mwezi Februari mwakani na matarajio yake ni kujiunga na timu yake mpya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad