HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 13, 2018

MKULIMA WA MIHOGO ASHINDA MILIONI 10 KUTOKA CBA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
BENKI ya Commercial Bank of Africa (CBA) kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom wamekamilisha rasmi leo kampeni yao  "Shinda na M pawa"  kwa kutangaza washindi watano waliojishindia bajaji na mshindi mkuu wa droo hiyo akijishindia pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni 10.

Akimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CBA Hakim Sheikh amesema kuwa benki hiyo inaendelea kutimiza ahadi kwa wateja wake kwa kuwazadia washiriki wote walioshiriki katika droo zote zilizofanyika.

Hakim amesema kuwa, "Kampeni hii imetupa fursa kubwa ya kuwahamasisha wateja wetu hasa kwa kujiwekea utamaduni wa kujiwekea akiba na tunawahimiza watanzania ambao bado hawajajiunga na benki ya CBA kujiunga na benki yetu ili waweze kufaidika na fursa mbalimbali zinazotolewa na benki ya CBA" ameeleza Hakim.

Hakim amesema kuwa benki yao itaendelea kutumia teknolojia katika katika kuhakikisha wanawafikia watanzania zaidi na kuongeza idadi ya wateja zaidi ya milioni 7 waliopo sasa.

Aidha amewapongeza washindi waliopatikana kwenye droo hiyo ya mwisho na kuahidi kudumisha  na kuboresha huduma yao na amewaomba watanzania waendelee kutumia huduma kutoka benki ya CBA.

Kwa upande wake Meneja masoko kutoka Vodacom Noel Mazoya amewapongeza benki ya CBA kwa kuendesha promosheni hiyo na uadilifu na wazi katika kuwapata washindi na hiyo imeleta mwamko mkubwa sana kwa wananchi kutumia huduma ya M pawa ili waweze kujishindia zawadi kutoka kwenye benki hiyo.

Mazoya amesema kuwa huduma ya M pawa imeletwa kwa lengo la kuwasaidia watu wa chini katika kuweka akiba zao na katika msimu huu wa sikukuu zaidi ya shilingi bilioni 1 zitatolewa kwa wateja wao wa Vodacom kupitia promosheni wanazoziendesha.

Pia amesema kuwa benki ya CBA na kampuni ya simu ya Vodacom wanafanya maboresho na wateja wategemee mambo mazuri kutoka kwao.

Katika droo hiyo ya mwisho bi. Sophia Sarapion (54) mkulima wa mihogo na mkazi wa Bukoba vijijini amejishindia pesa taslimu shilingi Milioni 10 huku bajaji 5 zikienda kwa; Abeid Abeid (28) mkazi wa Chalinze, Lucas Ngoye (28), Barawa Mariam (34) mkazi wa Kibamba, Msabila Hassan (40) mkazi wa Dar es Salaam na Mpela Hamis.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa benki ya CBA Hakim Sheikh akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya mwisho ambapo tangu kuanza kwa kuchezeshwa kwa droo hiyo jumla ya washindi 200 kwa kila droo wamepatikana.
Meneja masoko wa Kampuni ya simu ya Vodacom, Noel Mazoya akizungumza  na waandishi wa habari mara baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo ambapo ameipongeza benki ya CBA kwa kuendesha  shindano hilo kwa uadilifu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad