Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imeagiza amezitaka taasisi zote za na binafsi kuhakikisha wanajisajili kupitia Wakala Afya, Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) ili kutekeleza matakwa ya sheria. Hayo ameyasema Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Vijana na Ajira Jenista Mhagama alipowatembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa OSHA na kuangalia utendaji wao wa kazi katika kusimamia masuala aya usalama mahala pa kazi
Amesema uwepo wa taasisi ya OSHA ni muhimu kwa kuwa inalenga kuondoa dosari za aina mbalimbali hususani madhara katika maeneo ya kazi ambapo bila kufanya hivyo wafanyakazi wangekuwa waadhirika wakubwa katika sehemu za kazi zao.
“Taasisi zote na kampuni kujisajili na OSHA ili ziweze kufanya kazi kwa utaratibu wa kisheria, hii aina maana ina faida kwa Serikali, bali ni faida kwa taasisi , wafanyakazi wote kwa kuwa zaidi imelenga kuhakikisha inaondoa mazingira yote hatarishi ambayo pengine yangeweza kuleta madhara mahala Pa kazi ” amesema Mhagama.
Waziri Mhagama amaesema tangu kuanzishwa kwa chombo hicho kumekuwa na maendeleo ya usalama na afya za wafanyakazi yameweza kuonekana ambapo alisisitiza kuwa ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwa Wakala huyo ni taasisi zote hazina budi kuhakikisha zinajisajili.
Amesema katika kuhakikisha OSHA inafanya kazi zake kwa weledi na kuziwezesha taasisi mbalimbali kujisajili, tozo mbalimbali zilizokuwa zikitozwa kwa ajili ya usajili zimeondolewa, lengo likiwa kuzipunguzia mzigo taasisi hizo na kuzifanya zijisajili na wakala huyo kama ambavyo sheria ya Wakala wa Serikali Namba 30 ya Mwaka 1997 imeagiza.
Aidha aliitaka OSHA kuzidi kujihimarisha kiutendaji huku akiahidi kuwa Serikali itaendelea kuitazama kwa jicho la karibu ili iweze kutimiza malengo yake ya utendaji kawa weledi na kuamini kuwa kama wakala huyo akiwezeshwa ataweza kufanya kazi zake kwa weledi.
Mhagama amezipongeza alizipongeza taasisi mbalimbali za Umma zinazoendelea kuitikia wito wa sheria hiyo kwa kujisajili na Wakala huyo, akisisitiza kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kuondoa magonjwa, ajali na kuweka mazingira mazuri ya utendaji kwa taasisi hizo na hivyo kuongeza tija katika utendaji wa kazi.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Hajida Mwenda, mbali na kuainisha majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na wakala huyo, alisema tangu kuanzishwa kwake OSHA imezidi kupiga hatua na kufanikisha kuondoa vikwazo vilivyokuwemo katika utendaji wa taasisi mbalimbali.
Amesema katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwake,OSHA imezidi kupiga hatua mbalimbali na kufanikiwa kutoa elimu ya uelewa kwa wananchi, hatua iliyowezesha kuongeza wigo wa taasisi hizo kujisajili.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Vijana na Ajira Jenista Mhagama akizungumza na wafanyakazi wa Dawasa walioko katika mafunzo ya Ukimwi yanayoendeshwa na Wakala Afya, Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) wakati alipotembela ofisi za OSHA jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Hajida Mwenda akizungumza na waandishi habari kuhusiana na usimamizi wafanyakazi mahala pa kazi katika utoaji wa elimu wakati Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Vijana na Ajira Jenista Mhagama alipotembelea ofisi za OSHA jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Dawasa wakiwa katika mafunzo ya UKIMWI yanayoendeshwa na OSHA jijini Dar es Salaam.
afanyakazi wakiwa katika mkutano na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Vijana na Ajira Jenista Mhagama alipotembelea ofisi za OSHA jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment