HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 4 December 2018

MBWATE WACHOSHWA NA KERO YA UKOSEFU WA MAJI NA UMEME

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha 
WAKAZI wa mtaa wa Mbwate,kata ya Mkuza Kibaha Mjini mkoani Pwani, wanatatizo kubwa la ukosefu wa maji safi na salama ,hali inayosababisha kutumia maji ya kisima licha ya kuishi mjini. Aidha wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa nishati ya umeme ambapo tangu wawekewe nguzo ni takriban miezi nane bila muendelezo wowote.

Wakielezea kero zinazowakera ,akiwemo Kambangwa Kilema na Editha wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ,kata ya Mkuza, walisema inashangaza kutumia maji yasiyo salama kwa kushirikiana na ngedere. Alisema ,wanataabika na hali hiyo licha ya serikali kuahidi kumtua ndoo mama kichwani. 

"Sijui tuko mjini ya wapi, hatupishani na wanaoishi kijijini, hatuna maji salama, hatuna umeme, tunaiomba serikali ituangalie kwa jicho la tatu ili nasi tufaidike na huduma hizi muhimu "alifafanua Kilema. Hata hivyo, Kilema aliweka bayana juu ya changamoto ya ukosefu wa umeme, na kudai wamekuwa wakienda shirika la umeme Tanesco kuomba wasaidiwe lakini hakuna msaada wanaoupata. 
 Kufuatia changamoto hizo, Koka aliunda kamati iyohusisha na wananchi kwenda kufuatilia hatua zinazochukuliwa na DAWASA kuanza kusambaza maji pamoja na Tanesco kuhusu umeme ili kuondokana na shida hizo. Pamoja na hayo, Koka alisema ameshatoa kiasi cha sh. milioni tano kwa ajili ya kujenga madaraja madogo mawili katika miundombinu ya barabara mtaa wa Mbwate .
 Nae ofisa uhusiano na huduma kwa wateja Tanesco mkoani Pwani, Adrian Severin ,alisema mradi wa umeme unaopita Mbwate unahitaji nguzo zaidi ya 300. Alisema tatizo lilipo sasa ni upungufu wa upatikanaji wa vifaa ikiwa ni pamoja na nguzo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad