HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 18 December 2018

MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA TUNGUU WAKABIDHI SETI ZA JEZI KWA MICHUANO YA JIMBO CUP

 MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akizungumza na Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa Vya Michezo kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Jimbo hilo vilivyotolea na Mbunge na Mwakilishi kufanikisha michuano hiyo, hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni.
 MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akikabidhi Seti 10, zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo,kwa ajili ya Michuano ya Vijana ya Mpira wa Miguu wa  Jimbo la Tunguu Zanzibar. hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni.
 MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akimkabidhi Seti ya Jezi Mwenyekiti wa Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Ndg. Said Hassan, kwa ajili ya Michuano ya Vijana Mpira wa Miguu Jimbo la Tunguu, vilivyotolewa na Mbunge na Mwakilishi. kushoto Katibu wa Vijana wa Jimbo la Tunguu Ndg. Ali Khatib Kisu, hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni.
 MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akipata maelezo ya Bidhaa zinazotengenezwa na Vijana wa Kikundi cha Maendeleo cha Vijana Ubago Bi. Hawa Ali Mzee, akitowa maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na Vijana hao, akiangali Shampoo wakati akitembelea kikundi hicho,kushoto Mwenyekiti wa Vijana Jimbo la Tunguu Ndg.Said Hassan.
 MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said, akiangalia Shampoo inayotengenezwa na KIkundi cha Vijana cha Maendeleo Ubago, akipata maelezo kutoka kwa Katibu Hamasa wa Kikundi hicho Bi. Hawa Ali Mzee, wakati alipotembelea kikundi hicho Dunga Bweni Wilaya ya Kati Unguja.
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akiangalia moja ya nguo zinazozonwa na Kikundi cha Vijana na Maendeleo Ubago, wakati alipowatembelea Vijana hao katika Kituo chao kuangalia shughuli wanazozifanya za utengenezaji wa Shampoo, Sabuni. Lotion na mafuta ya mgando na ushoni wa nguo.(Picha na Othman Maulid)

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad