HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 15 December 2018

KATIBU MKUU DOTO:SERIKLI INATAMBUA MCHANGO WA TIA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema kuwa inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)katika kuandaa watalaam wa Tasnia ya Uhasibu, Ununuzi na Ugavi Biashara pamoja na uongozi wa Rasilimali Watu.

Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James wakati alipomwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango  katika mahafali ya 16 ya Taasisi Uhasibu Tanzania  kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam.

James amesema kuwa serikali itaendelea kuunga mkono pamoja na taasisi kutekeleza majukumu kwa weledi katika kubuni mbinu mpya za  kuimarisha mapambano ya kupata mafanikio makubwa.
Amesema Taasisi hiyo iendelee kubuni mbinu kujitangaza zaidi na kujiuza kwa bidhaa wanazozitoa kwa ndani na nje nchi katika ili  kuongeza  wanachuo zaidi.

Aidha amesema TIA iongeze jitihada za kufanya taifaiti mbalimbali, kutoa ushauri wa kitaalam  katika maeneo mbalimbali ya uhasibu, ugavi na ununuzi , biashara na Rasilimali watu katika kuongeza mapato kwa kasi

“Sera kwa sasa ni uchumi wa viwanda hivyo wazalishwe watalaam wenye umahiri ili kufanikisha azima ya serikali ya Tanzania ya viwanda katika kukabiliana na changamoto za mapato na matumizi ya fedha za Umma”amesema James

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt Joseph Kihanda amesema kuwa katika kuhtimu wanafunzi 4022 wamepita katika changamoto mbalimbali. Amesema kuwa chuo kinachangamoto ya eneo pamoja na wahadhiri na kuitaka serikali kuangalia namna ya kuweza kuwasaidia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza katika mahafali ya 16 ya Taasisi Uhasibu Tanzania (TIA)  kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa TIA, Wakili Said Chiguma akizungumza kuhusiana na hali ya uendeshaji wa Taasisi hiyo katika mahafali ya 16 ya Taasisi Uhasibu Tanzania (TIA)  kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)Dkt. Joseph Kihanda akizungumza historia ya taasisi hiyo mahafali ya 16 ya Taasisi Uhasibu Tanzania (TIA)  kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam
Wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania  (TIA) katika  mahafali ya 16 ya Taasisi hiyo   kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wakicheza muziki baada ya kutunukiwa shahada mbalimbali zinazotolewa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania  (TIA)katika katika  mahafali ya 16 ya Taasisi hiyo   kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad